Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-25 14:46:13    
Jukumu la kwanza la kazi ya maji nchini China ni kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa

cri

Maji ni chanzo cha maisha. Tarehe 22 March ni siku ya mwaka wa 13 ya maji duniani, kauli mbiu ya siku hiyo ni "maji kwa maisha". Mtaalamu wa wizara ya maji ya China alifahamisha kuwa, wizara hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kuhifadhi vyanzo vya maji na kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa kwa wananchi wa China.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa, kila mwaka majitaka zaidi ya tani bilioni 400 yanatolewa duniani, ambayo yanachafua zaidi ya tani trilioni tano za maji, na kusababisha watu milioni kadhaa duniani kufa kutokana na maradhi yanayosababishwa na kunywa maji machafu. Data zilizotolewa na wizara ya maji ya China zimeonesha kuwa, nchini China watu zaidi ya milioni 300 wanatumia maji yasiyo salama, magonjwa yanayosababishwa na maji machafu, kuchafuka kwa chanzo cha maji ya kunywa, wadudu aina ya "kichocho", ukosefu wa maji kufuatana na majira na masuala mengine bado yapo katika sehemu kadhaa.

Mtaalamu huyo alisema kuwa, ili kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa na kulinda afya za wananchi wa China, katika miaka mitano iliyopita, serikali ya China kwa jumla ilitenga yuan bilioni 18 kujenga miradi zaidi ya laki nane ya maji ya kunywa vijijini, ambayo imewanufaisha wanavijiji zaidi ya milioni 57.

Wakati huo huo, ili kutatua vizuri masuala yanayohusu usalama wa maji, wizara ya maji ya China inafanya kazi nne.

Kwanza, kubainisha hali ya usalama wa maji ya kunywa na kuweka mpango wa ujenzi wa usalama wa maji ya kunywa. Wizara ya maji ya China sasa iko mbioni kutunga "mpango wa ujenzi wa usalama wa maji ya kunywa katika miji na vijiji kote nchini", na kufanya kwa kina sensa kuhusu usalama wa maji.

Pili, kutenga fedha nyingi zaidi katika ujenzi wa miradi ya usalama wa maji ya kunywa, na kuweka sera ya kipaumbele katika matumizi ya ardhi, umeme, ushuru na sekta nyingine kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa miradi hiyo.

Tatu, kushughulikia vizuri kazi ya ujenzi wa usalama wa maji ya kunywa. Idara husika zinatakiwa kuweka sehemu ya hifadhi ya vyanzo vya maji ya kunywa na eneo la usimamizi wa miradi ya maji, kutunga sheria husika ili kuzuia kuchafuka kwa vyanzo vya maji na uharibifu wa binadamu. Kuimarisha upimaji na usimamizi wa ubora wa maji, na kuboresha mfumo wa usimamizi wa usalama wa maji ya kunywa.

Nne, kufanya mageuzi kwa kina, kuboresha mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji ya kunywa ili kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa kwa wananchi na kuboresha huduma za maji.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-25