Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-28 16:34:42    
Harakati za sayansi na teknolojia dhidi ya Ukimwi zaanzishwa mikoani Henan na Yunnan nchini China

cri

Harakati za sayansi na teknolojia dhidi ya Ukimwi zimeanzishwa mikoani Henan na Yunnan nchini China. Harakati hizo zinaongozwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirkisha Wizara ya Afya na Idara ya Taifa ya Udhibiti wa Madawa. Naibu waziri wa sayansi na teknolojia Bw. Li Xueyong alisema kuwa harakati hizo zinalenga kuinua upeo wa sayansi na teknolojia katika kinga na tiba ya Ukimwi, ili kupunguza haraka idadi ya watu wanaoambukizwa na wanaokufa kutokana na Ukimwi.

Bw. Li Xueyong alisema, Ukimwi ni ugonjwa wa kuambukiza haraka na unaleta madhara makubwa kwa uchumi. Tokea mwaka 1985 mgonjwa wa kwanza alipogunduliwa, maambukizi yake ni ya haraka sana nchini China, hasa katika mikoa ya Henan na Yunnan, kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo ni ngumu.

Ili kukidhi mahitaji ya haraka ya kukinga na kutibu Ukimwi harakati hizo zimetilia mkazo katika kazi nne:

Moja ni kutafiti na kupata elimu kuhusu maambukizi ya Ukimwi. Utafiti huo utagundua aina tofauti za maambukizi katika sehemu tofauti na aina tofauti ya maambukizi miongoni mwa makundi tofauti ya watu, hali tofauti ya wagonjwa walipokuwa mwanzoni mwa ugonjwa, ili kutabiri na kukatisha maambukizi. Pili ni utafiti kuhusu tiba. Uchunguzi utafanywa katika tiba ya mchanganyisho ya Kichina na ya Kimagharibi, kuchuja aina bora za matibabu, na kupunguza athari mbaya ya dawa. Tatu ni kufanya utafiti wa chanjo, hasa chanjo ya kinga, kufanya uchunguzi ili kupata madawa yaliyo bora na yenye athari mbaya kidogo na kupata madawa ya kimaumbile na madawa ya mitishamba. Nne kuanzisha sehemu ya kufanyia utafiti huo kama ni mfano wa kuigwa nchini China. Utafiti wa sayansi na teknolojia katika kinga na tiba katika mikoa hiyo miwili utakuwa ni kama mfano wa uchunguzi wa sayansi na teknoljia dhidi ya Ukimwi nchini China.

Bw. Li Xueyong alisema, harakati hizo zinatilia mkazo katika matumizi ya dawa za Kichina na kujitahidi kujaribu kupata aina tofauti za kinga na tiba kwa kushirikiana na nchi nyingine. Pamoja na hayo ushirikiano na nchi za nje utaimarishwa ili kupata uzoefu wa nchi hizo katika kusukuma mbele kazi ya kupambana na Ukimwi nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-28