Mkutano wa siku 2 wa "Baraza la Maendeleo ya China" umefungwa hivi karibuni hapa Beijing. Kuweza kudumisha maendeleo ya kasi kwa uchumi wa China, kulikuwa moja ya suala linalofuatiliwa na watu. Wanauchumi mashuhuri wa nchini na wa kigeni walioshiriki kwenye mkutano huo walisema kuwa nchini China kuna nguvu kubwa inayohimiza maendeleo ya kasi na endelevu. Waliongeza kuwa China ina uwezo kabisa wa kudumisha 8% ya ongezeko la uchumi katika miaka kadhaa ijayo.
"Baraza la Maendeleo ya China" lilianzishwa na kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali miaka mitano iliyopita. Mkutano unaofanyika kila mwaka wa baraza hilo, ni moja ya sehemu ya kufanya mazungumzo kati ya serikali ya China na wanauchumi mashuhuri wa duniani. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu wa baraza hilo ilikuwa ni "China iliyoko katika mfumo wa uchumi wa dunia". Maofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya China, wawakilishi wa mashirika duniani viongozi wa kampuni mashuhuri za kimataifa pamoja na wanauchumi mashuhuri wa nchini na wa nje wapatao zaidi ya 100 kwa jumla walishiriki kwenye mkutano huo wa mwaka.
Katika miaka zaidi ya 20 ya karibuni, uchumi wa China umekuwa ukidumisha ongezeko la asilimia 9 na kufanya China kuwa moja ya nchi zenye ongezeko kubwa la uchumi duniani. Jumuiya ya kimataifa inaona kuwa umuhimu wa maendeleo ya uchumi ya China wa kuhamasisha uchumi wa dunia umeimarika siku hadi siku, na ongezeko la uchumi wa China limekuwa moja ya nguvu inayochangia ongezeko la uchumi wa dunia. Hivyo, kuweza kudumisha maendeleo makubwa na mwafaka au la kwa uchumi wa China kulikuwa moja ya masuala nyeti yaliyozungumziwa na wanauchumi mashuhuri wa China na wa nchi za kigeni walioshiriki kwenye mkutano wa mwaka huu.
Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali Bw. Sun Xiaoyu alisema kuwa, katika miaka ya karibuni uchumi wa China umeingia kipindi kipya cha ongezeko kubwa kutokana na kuinuka kwa kiwango cha ununuzi vitu wa wakazi nchini China, kuharakishwa kwa mchakato wa ujenzi wa viwanda na kuongezeka kwa miji. Anaona kuwa katika kipindi cha siku za baadaye, mambo hayo yataendelea kuwa nguvu kubwa inayodumisha maendeleo ya kasi ya uchumi wa China. Alisema,
"Katika miaka 5 hadi 15 ijayo, kuharakishwa kwa ujenzi wa viwanda na kuongezeka kwa idadi ya miji nchini China, ujenzi wa miundo-mbinu wa mijini utaendelezwa katika maeneo makubwa, ambao utaleta mahitaji makubwa ya wakazi. Uchumi wa China utakuwa na uwezo kabisa wa kudumisha ongezeko kubwa kwa kutegemea masoko makubwa ya nchini, rasilimali kubwa ya nguvu-kazi, kiasi kikubwa cha akiba ya fedha za wakazi kilichowekwa benkini, hamasa ya jamii inayoletwa na mageuzi na kutegemea uvumbuzi wa teknolojia."
Bw. Sun alisema kuwa kwa kawaida, upungufu wa mitaji ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi zinazoendelea, lakini baada ya kuwa na maongezeko makubwa ya uchumi katika miaka miongo kadhaa iliyopita, pato la taifa la China limechukua nafasi ya 7 duniani ikiwa ni nchi yenye akiba ya fedha za kigeni kinacholingana na nchi za dunia ya pili. Aidha, hivi sasa China ni moja ya nchi yenye kivutio kikubwa cha uwekezaji duniani, hivyo tatizo la mitaji inayohitajiwa kwa maendeleo ya siku za baadaye ya China imetatuliwa kwa jumla. Mbali na hayo, kuharakishwa kwa kuongezeka kwa idadi ya miji kutahimiza kupanuka kwa uwekezaji na ununuzi wa vitu, ambapo kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji pia kutahamasisha uwekezaji binafsi wa wakazi wa China, mambo ambayo ni nguvu kubwa inayohamasisha ongezeko la kasi la uchumi wa China.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya HSBD HOLDING PLC Bw. John Bond anaona kuwa katika miaka mitano iliyopita uchumi wa China ulipata maendeleo makubwa, tena pamoja na kuharakishwa kwa hatua za mageuzi, uchumi wa China utaweza kudumisha kasi ya ongezeko. Alisema,
"Mwaka huu ni wa mwisho wa mpango wa 10 wa maendeleo ya miaka mitano, katika miaka mitano hiyo iliyopita uchumi wa China ulidumisha ongezeko kubwa la uchumi la kushangaza, ambapo pia ilifaulu kudhibiti ongezeko kubwa la uchumi la kupita kiasi. Serikali ya China imenuia kukabilia changamoto mpya katika mpango wa maendeleo ya miaka mitano unaofuata."
Ingawa wanauchumi mashuhuri wana imani kuhusu maendeleo ya uchumi wa China, lakini wameeleza kuwa maendeleo ya uchumi wa China bado yanakabiliwa na matatizo mengi, ambayo endapo hayatatatuliwa vizuri lengo la maendeleo ya kasi ya uchumi, huenda halitaweza kutimizwa.
Naibu waziri mkuu wa China Zeng Peiyan alipotoa hotuba kwenye mkutano huo kuhusu namna ya kutatua matatizo hayo, alisema,
"Maendeleo ya uchumi wa China yanakabiliwa na vikwazo vinne vikiwa ni pamoja na upungufu wa rasilimali; shinikizo linalotoka kwenye hifadhi ya mazingira; kupanda kwa gharama ya nguvukazi na uwezo duni wa uvumbuzi wa teknolojia."
Wanauchumi wanaona kuwa athari ya maendeleo ya uchumi wa China kwa dunia inaongezeka kwa mfululizo, ambayo inatoa soko na nafasi kubwa kwa nchi nyingine duniani.
Picha Husika>>
1 2
|