Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-31 20:02:59    
Maisha ya furaha ya watu wanaotoka Amerika ya kaskazini mjini Tianjin

cri

Bw. Cameron na mkewe Bi.Shelly ni wa-Canada, ambao walifika Tianjin miaka miwili iliyopita kuwa walimu wa lugha ya Kiingereza katika sekondari ya Binhai. Kabla ya kuja China walikuwa na wasiwasi kidogo kuhusu jinsi ya kuzoea maisha ya Tianjin kutokana na tofauti ya mazingira ya kiutamaduni na kimaisha. Bw. Cameron alisema kwa furaha kuwa, baada ya kufika Tianjin aliona kuwa, mazingira ya kazi na maisha ya huko ni mazuri zaidi kuliko walivyofikiria. Maduka makubwa na mikahawa iko kila mahali, hospitali na shule za kisasa zinafanana na zile za maskani yao Ottawa.

"Jambo la kwanza linalonifurahisha ni kuwa, asubuhi ya siku ya kwanza baada ya kufika Tianjin tutalipotembelea nje, takaona bustani kubwa yenye miti mingi na majani, watu wengi walikuwa wanafanya mazoezi kwenye bustani hiyo, tulijisikia vizuri sana."

Maisha ya Bw. Cameron na Bi. Shelly ni mazuri. Kila baada ya kazi, hufanya matembezi bustanini, au kufanya mazoezi katika jumba la kujenga mwili, au kunywa kahawa katika mikahawa ya "star bucks". Lakini wanapenda zaidi kula chakula kitamu cha Tianjin. Mji wa Tianjin uko karibu na pwani, kuna vitoweo vya aina mbalimbali vya samaki vilivyopikwa kwa njia ya kichina, ambayo vinawafurahisha sana.

Bwana Cameron anajua kupiga gitaa, filimbi na ala nyingine, hivyo kila baada ya kazi, yeye hupenda kupiga ala pamoja na mke wake.

Bw. Michael J. Layden kutoka Marekani pia anapenda sana kuishi Tianjin, mji wenye vivutio vikubwa. Bw. Layden mwenye umri wa miaka 50 mwaka huu anapenda kukusanya stempu za nchi mbalimbali. Miaka zaidi ya 10 iliyopita, alikutana na msichana wa China Xu Zhongyu aliyekuwa anasoma Hawaii. Alifurahi sana Alipoambiwa kuwa Xu Zhongyu ni mkazi wa Tianjin, kwa sababu alijua kuwa Tianjin ni chanzo cha posta ya China.

Bw. Layden alimwoa Xu Zhongyu na kuja China kumfuata mke wake mwaka 1991, na kuamua kuishi huko. Katika miaka ya hivi karibuni Bw. Layden amekusanya stempu elfu kumi hivi kuhusu Tianjin. Wakati alipokusanya stempu alianza kupenda utamaduni na historia ya Tianjin. Alisema:

"Historia ya stempu inaeleza hadithi za maisha ya binadamu. Unaweza kufahamu hadithi zilizowahi kutokea kutoka kwenye barua zilizowekwa ndani ya bahasha. Nimefahamu mambo mengi kuhusu Tianjin baada ya kufanya utafiti kuhusu historia ya stempu ya Tianjin. Kadiri nilivyofahamu mambo ya Tianjin, ndivyo nilivyoona umuhimu wa hadhi ya Tianjin katika historia ya maingiliano kati ya China na nchi za nje."

Mwaka 2001, Bw. Layden alichapisha kitabu cha kwanza kuhusu stempu, bahasha, kadi za posta maarufu zaidi ya 600 alizozikusanya. Kitabu hicho kilishiriki kwenye maonesho ya stempu yaliyofanyika nchini China, Marekani, na Thailand na kupata tuzo mara kadhaa. Hivi sasa ujuzi wa Bw. Layden kuhusu historia ya Tianjin, ni mkubwa kuliko wa wakazi wengi wa Tianjin.

Bw. Layden alisema kuwa, atajitahidi kadiri awezavyo kuwafahamisha watu wa duniani mambo ya Tianjin. Mwaka jana alichapisha kitabu cha pili.

Msichana Wilson kutoka New York, Marekani mwaka huu ana umri wa miaka zaidi ya 20. Aliwahi kufika China alipokuwa mwanafunzi wa sekondari, ukuta mkuu na kasri la wafalme yalimpa picha nzuri sana, hivyo ana hamu ya kufahamu zaidi kuhusu historia na ustaarabu wa China. Miaka miwili iliyopita, mara baada ya kuhitimu masomo kutoka chuo kikuu nchini Marekani, Bi. Wilson alikuja China kufanya kazi katika nyumba ya watoto ya Tianjin.

Katika nyumba ya watoto, Bi. Wilson aliwashughulikia kwa makini watoto wote wasiojiweza, kutathmini magonjwa yao na kutunga mpango kwa kufufua afya zao.

"Nashughulikia mambo ya watoto wa nyumbani hiyo, sifahamu baadhi ya magonjwa waliyonayo, nawapeleka watoto hao kuonana na daktari, au kununua vitu dukani. Hayo yote yameongeza uzoefu wangu wa kimaisha."

Kadiri Bi. Wilson alivyoishi mjini Tianjin, ndivyo alivyoupenda mji wa Tianjin na watoto wa huko. Kila alipowazungumzia watoto hao, alionekana mwenye furaha usoni.

Bi. Wilson anawapenda watoto wa nyumba ya watoto wa Tianjin, watoto hao pia wanampenda yaya huyo mgeni kutokana na uzuri wake na kuwafundisha jinsi ya kucheza michezo na kucheza dansi.

Bi. Wilson ameshazoea maisha ya Tianjin. Yeye si kama tu anapenda kula chakula cha kichina, bali pia anajifunza namna ya kupika vitoweo vya kichina, na kuwaalika marafiki zake kuonja vitoweo alivyopika. Anakwenda kazini kwa kupanda baiskeli, licha ya kujifunza kichina, yeye pia anawafundisha Kiingereza walimu wa nyumba ya watoto.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-31