China ni nchi yenye eneo kubwa, hivyo mazao ya majini ni ya aina nyingi tena uzalishaji wake ni mkubwa. Sekta hiyo ni sekta yenye mustakabali mzuri wa maendeleo. Kwa ujumla mazao ya majini nchini China yanaweza kugawanywa kuwa ya aina tano, yaani samaki, samakigamba, moluska, mwani na mamalia. Samaki ni aina muhimu kabisa katika aina hizo za mazao ya majini. China ina aina 2400 za samaki kati ya aina 3000 samaki waliopo duniani, na miongoni mwa aina hizo, samaki wa baharini wanachukua asilimia 60. Mwaka 1990 uzalishaji wa mazao ya majini nchini China ulifikia tani milioni 12.18, na kushika nafasi ya tatu duniani. Mazao ya majini ya China pia yanaweza kugawanywa katika aina tatu kwa mujibu wa maeneo tofauti, yaani mazao ya baharini, mazao katika maeneo ya bahari ya karibu baharini na mazao ya bara.
1. Mazao ya baharini:
Uzalishaji wa mazao ya baharini unachukua asilimia 57.72 ya uzalishaji wa mazao yote ya majini. Miongoni mwa uzalishaji huo, uzalishaji wa samaki ni mkubwa kabisa. China ina aina zaidi ya 1700 za samaki wa baharini, miongoni mwa aina hizo, kuna aina 300 za samaki wa biashara ambazo aina 60 hadi 70 ni za aina za kawaida. Aidha, kuna aina zipatazo 2000 za mwani, aina zipatazo 300 za kaa na kamba, aina zipatazo 200 za moluska. Katika bahari ya Manjano na bahari ya Bo kuna aina zaidi ya 250 za samaki, na uzalishaji wa samaki huko unachukua asilimia 27.9 ya uzalishaji wote. Katika bahari ya Mashariki kuna aina zaidi ya 440 za samaki, na uzalisaji unachukua ailimia 51.8, hivyo bahari hiyo inasifiwa kuwa ni hazina ya samaki. Na katika bahari ya Kusini kuna aina zipatazo elfu 1 za samaki, lakini uzalishaji si mkubwa, ambao unachukua asilimia 20.3 ya uzalishaji wote nchini China.
Mazao katika maeneo ya baharini ya karibu
Kutokana na uvuvi wa kupita kiasi wa miaka mingi, maliasili ya majini katika sehemu hiyo imepungua mwaka hadi mwaka. Miaka ya karibuni, China imechukua hatua za kufuga samaki wadogo na kuweka majabari yanayotengenezwa na binadamu kwa lengo la kuboresha mazingira mazuri kwa maisha ya samaki, na hatua hizo zimepata maendeleo kadha. Hivi sasa kuna aina 60 za samaki, kamba, samakigamba na mwani zinazofugwa na binadamu nchini China. Mwaka 1990 uzalishaji wa mazao yanayofugwa na binadamu baharini nchini China umefikia tani milioni 1.624 ambao unachukua nafasi ya kwanza duniani.
Mazao ya bara
China ni nchi yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya majini kwenye nchi kavu. Kuna aina zaidi ya 800 ya samaki katika mito na maziwa, miongoni mwao samaki muhimu wa kibiashara ni zaidi ya 40. Uzalishaji wa mazao hayo unachukua asilimia 10 ya mazao ya aina hiyo duniani. Na katika uzalishaji huo, uzalishaji wa kamba, kaa na samakigamba unachukua asilimia 3.2 tu. Samaki wa herring, grass carp, chub na Bighead carp ni samaki muhimu kabisa wa maji baridi nchini China.
Idhaa ya Kiswahili 2005-03-31
|