Hivi karibuni Beijing ilipopanga mpango mpya kuhusu maendeleo yake katika siku za usoni, ilitoa lengo jipya la kuujenga mji huo kuwa mji unaofaa kwa maisha ya watu. Hatua hii imefuatiliwa na watu wengi.
Tarehe 27 Januari mwaka j2005, Baraza la serikali la China liliidhinisha rasmi "Mpango wa jumla wa mji wa Beijing (mwaka 2004 hadi 2020). Mpango huo umethibitisha lengo la mji wa Beijing la "mji mkuu wa taifa, mji wa kimataifa, mji maarufu wa utamaduni na mji unaofaa kwa maisha ya watu".
Katika mpango huo, lengo la "mji unaofaa kwa maisha ya wakazi" kwa mara ya kwanza limevutia watu macho.
Naibu mkurugenzi wa Kamati ya mipango ya Beijing Bwana Tan Xuxiang alisema kuwa, watu waliojadili walikuwa na mabishano kuhusu kuweka au la lengo la "kituo cha uchumi", lakini hatimaye halikuandikwa, lakini hii haimaanishi kuwa Beijing haitakuwa kituo cha uchumi, kwani kituo cha uchumi kwa kawaida ni uwezo ulio nao mji mkuu wa taifa au mji mkuu wa mkoa, haina haja kusisitiza tena.
Mpango wa jumla wa mji wa Beijing wa mwaka 1991 hadi 2010 ulioidhinishwa mwaka 1993 na Baraza la serikali la China uliotekelezwa miaka iliyopita, malengo mengi ya maendeleo kwenye mpango huo yamekamilika kabla ya wakati. Lakini matatizo mengi mapya yamejitokeza siku hadi siku: msongamano wa kupita kiasi unaonekana katika sehemu ya katikati ya mji, hasa hali ya msongamano wa magari ni mbaya siku hadi siku, uchafuzi wa mazingira bado ni mbaya, na shinikizo la hifadhi ya mji maarufu wa historia na utamaduni wa Beijing ni kubwa sana. Maendeleo ya uchumi na jamii ya Beijing yanakabiliwa na vikwazo vingi.
Hivi sasa ujenzi wa Beijing unapaswa kufanyika kwa mpango wa kisayansi, lengo la kuujenga kuwa mji unaofaa kwa maisha ya wakazi ni mwelekeo mpya wa maendeleo.
Kujenga mji wa Beijing kuwa mji unaofaa kwa maisha ya wakazi kunatakiwa kujenga mazingira ya afya, kuwa na huduma rahisi, kuongeza nafasi nyingi za ajira na kuwa mji wenye usalama.
Kutokana na mpango huo, katika miaka kadhaa ijayo, Beijing itajenga miji midogo ya aina mpya pembezoni mwake, kila mji mdogo utakuwa na watu zaidi ya laki 5, na miji hiyo itakuwa na nguzo za kazi, na mfumo kamili wa ajira, hospitali, shule, maduka, posta na mikahawa. Ifikapo mwaka 2020, idadi ya jumla ya watu wa Beijing itafikia milioni 18, ambapo idadi ya watu wa kiini cha mji wa Beijing itapungua kuwa milioni 5.4 kutoka milioni 6.5.
Kutokana na mpango mpya, muundo wa nafasi za Beijing utafanyiwa marekebisho makubwa. Sehemu za wilaya mbalimbali Beijing zitajengwa kuwa sehemu za aina mbalimbali za mazingira mazuri ya viumbe, usitawi wa shughuli za teknolojia za hali ya juu, kituo cha michezo ya Olimpiki na kituo cha biashara.
Beijing itaendeleza uchumi wa viwanda vya aina mpya vya shughuli zenye sayansi na teknolojia za hali ya juu, matumizi machache ya nishati, uchafuzi kidogo kwa mazingira ambapo wataalamu wanaweza kuonesha umuhimu wao ipasavyo.
Mji mkubwa wa kisasa hakika unapaswa kuwa mji unaofaa kwa maisha ya wakazi. Mpango mpya wa Beijing utauwezesha mji huo uendelee haraka na vizuri.
Idhaa ya kiswahili 2005-04-01
|