Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-08 18:29:50    
Muziki wa kale wa Dunhuang

cri

Mwanzoni mwa karne hii, kitabu cha ajabu kiligunduliwa ndani ya pango la kuhifadhi misahafu huko Dunhuang, mkoani Gansu. Maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho yalikuwa hayasomeki vizuri, kwa hivyo, wataalamu wengi walishindwa kuelewa kilichoandikwa. Baada ya miaka 90, kutokana na juhudi za wataalamu, ilithibitishwa kwamba kitabu hiki ni cha muziki na ngoma zilizofuatana na upigaji wa kikanda cha pipa ambayo ni aina ya vinanda vya kale vya China. Kitabu hiki kilinakiliwa kwa mkono wakati wa karne ya tisa, hiki ni kitabu cha zamani duniani.

Ni miaka ya hivi karibuni tu ilipowezekana kwa kitabu hicho kutafsiriwa. Mwishoni mwa mwaka 1991, Bw. Xi Zhengguan, mtaalamu mashuhuri wa historia ya Dunhuang, na Mkurugenzi wa Jumba la Sanaa la Dunhuang alifanikiwa kutafsiri kitabu hicho cha mafumbo chenye nyimbo 25 za muziki wa Enzi ya Tang (618-907) baada ya utafiti mgumu wa miaka 10. Muziki uliopotea kwa muda wa miaka 1,000 ukawa umerudia tena uhai wake, jambo hilo liliishtusha dunia kwelikweli.

Wasanii wa Jumba la Sanaa la Dunhuang wamekuwa wakivuma sana kwa kuwa walifanikiwa kucheza mchezo wa ngoma iitwao "Maua kwenye Njia ya Hariri". Sasa, wasanii hao wametunga mchezo mwingine wa ngoma uitwao "Muziki wa Kale wa Dunhuang" kutokana na kitabu kilichotafsiriwa na Xi Zhenguan. Mchezo huo umechanganya vema mashairi, muziki na ngoma.

"Muziki wa Kale wa Dunhuang" unatumia ala za muziki zilizotengenezwa kwa kuingia ala zile za Enzi ya Tang; unapiga muziki wa kale wa Dunhuang, kuimba nyimbo zilizotungwa kwa mujibu wa mashairi ya kale ya Dunhuang na kusimulia hadithi zilizoelezwa kwenye michoro ya kutani, kama vile watu wanajumuika kujiburudisha; tamasha kubwa ya kupiga kikanda cha pipa ya familia laki moja za kabila la Wahu; askari wa kulinda mpaka wa taifa wenye dereya wakiwa wamelala jangwani baada ya kulewa; malaika wanauke kwa wanawame wakijiburudisha peponi. Mchezo huo unadhihirisha vema maisha ya jamii na utamaduni wa Enzi ya Tang pamoja na tabia na mila za raia wake.

Ngoma ya "Muziki wa Kale wa Dunhuang" inavutia macho, miondoko yake mingi na hisia za nyuso za wahusika imebuniwa kutokana na wachezaji ngoma wa kwenye michoro. Kwenye jukwaa, wachezaji wenyewe wanapiga viande vya muziki huku wakiimba na kucheza ngoma. Wanabendi wa bendi wakivalia mavazi ya Kitang wanaonekana jukwaani vilevile wakipiga filimbi. Aina moja ya muziki huu ina utamu wa pekee na ni nyororo; aina nyingine ni ya kivita yenye kuonyesha ushupavu na ukakamavu. Ukiwa unaendana vizuri na mashairi na michoro ya kutani ya Enzi ya Tang, mchezo wa "Muziki wa Kale wa Dunhuang" umedumisha sifa za enzi hiyo na kuzitukuza zaidi.

Jumba la Sanaa la Dunhuang limefanya kazi kubwa ya kufufua na kuchanganya mashairi, muziki na ngoma vilivyopotea kwa miaka elfu moja. Kwa mara nyingine, onyesho la "Muziki wa Kale wa Dunhuang" limeishangaza dunia nzima.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-08