Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vimedumu kwa miaka 14. Ili kukomesha mapambano na kurejesha amani nchini humo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 1509 tarehe 19 mwezi Septemba mwaka 2003, na kuamua kupeleka wanajeshi wa kulinda amani nchini Liberia. Kutokana na ombi la Umoja wa Mataifa, serikali ya China ilipeleka wanajeshi 275 wa uhandisi nchini Liberia mwaka 2004. Wanajeshi hao walijenga barabara, madaraja na vituo vya wanajeshi nchini Liberia kwa muda wa mwaka mmoja.
Wanajeshi hao wa China walianza kazi mara tu baada ya kufika nchini Liberia . Kutokana na vita vya muda mrefu, barabara na madaraja nchini Liberia yameharibika vibaya. Ili kuhakikisha utekelezaji wa kazi za Umoja wa Mataifa za kunyang'anya silaha kutoka kwa wanamgambo waliokuwa wanapambana, barabara na madaraja hayo yalipaswa kujenga upya. Lakini mwezi Aprili mwaka huo, Liberia iliingia majira ya masika. Hali hiyo ilileta matatizo katika ujenzi wa barabara na madaraja. Hata hivyo, wanajeshi wa China waliipokea kazi hizo ngumu wakati wanajeshi wa nchi nyingine walikataa kuifanya.
Katika majira ya masika, ingawa walikabiliwa na jua kali na mvua mkubwa, lakini wanajeshi wa China hawakuwa na malalamiko yoyote. Baada ya kazi ngumu ya miezi minne, wanajeshi hao wa China walikamilisha ujenzi wa madaraja 19 na barabara zenye urefu wa kilomita 527. Juhudi za wachina ziliwezesha kazi ya Umoja wa Mataifa za kunyang'anya silaha kutoka kwa wanamgambo wanaopambana. Kamanda mkuu wa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa aliwasifu kuwa, wanajeshi wa China walifanya muujiza, na kutoa mfano mzuri kwa wanajeshi wa nchi nyingine.
Mbali na kazi za kawaida za ujenzi, wanajeshi wa China mara kwa mara walitoa misaada mbalimbali kwa wenyeji wa huko. Vitendo vyao vilizidisha urafiki na maelewano kati ya China na Afrika.
Usiku wa tarehe 10 mwezi Juni mwaka 2004, kundi moja la wanajeshi wa China waliokuwa wakijenga barabara huko Riverside walikuwa wamelala usingizi baada ya kazi za kuchosha za siku nzima. Ghafla king'ora kililia, mlinzi akasema kwamba nyumba moja ya kijiji kilichoko mita 500 na kituo chao ilikuwa imechomwa moto, na moto huo ulienea na kuteketeza nyumba nyingine kijijini kutokana na upepo mkali. Ingawa ilikuwa hatari kwa wanajeshi hao wachina kuondoka kutoka kwenye kituo cha kijeshi usiku, lakini hawakurudi nyuma. Baada ya dakika tano tu, wanajeshi wote wa kituo hicho walifika kwenye sehemu ulipotokea moto. Kutokana na wanakijiji wengi kuwepo barabarani, magari hayakuweza kuingia, wanajeshi hao walilazimika kuzima moto kwa mabeseni yaliyojaa maji. Baada ya kazi ya uokoaji iliyofanyika kwa saa mbili, hatimaye moto ulizimwa. Wanakijiji waliwashukuru sana kazi ya uokoaji ilifanywa na wanajeshi wa China. Baadhi yao walisema neno la kichina Xiexie ambalo maana yake ni Asante ili kuonesha shukrani zao kubwa.
Wanajeshi wa China walipata shukrani za watu wa Afrika baada ya kazi ya kuokoa moto, hivyo wamejipatia heshima na marafiki waafrika baada ya kuokoa maisha ya maelfu ya watu yaliyohatarishwa na gesi ya sumu.
Tarehe 20 mwezi Juni mwaka 2004, mitungi miwili mikubwa ya kuwekea gesi ya chlorine katika kituo kimoja cha kusafisha maji, kilichoko kilomita 4 na katikati ya mji wa Zwedru ilipasuka, na gesi ya sumu ilianza kuvuja. Eneo lenye kilomita moja ya mraba ikawa sehemu isiyo na viumbe vilivyoko hai, na eneo hilo lilikuwa likizidi kuongezeka. Watu zaidi ya 2000 walioishi karibu na sehemu hiyo walilazimika kuhama makazi yao, na baadhi yao waliumwa kutokana na gesi ya sumu.
Kutokana na nidhamu ya Umoja wa Mataifa, kazi za wanajeshi wa uhandisi wa China nchini Liberia zilikuwa kujenga barabara tu, madaraja na vituo vya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Lakini wakati watu wa Afrika walipokabiliwa na hatari kubwa, wanajeshi hao wa China hawakusita hata kidogo kuwasaidia. Tarehe 21 alasiri, kikundi cha wanajeshi 35 wachina wa kuokoa maafa kilipelekwa kwenye kituo hicho cha maji. Wanajeshi hao kwanza waliziba kabisa ile mitungi iliyopasuka, ili kuzuia kutoka kwa gesi ya sumu. Kisha walibeba mitungi hiyo miwili iliyojaa gesi ya sumu mabegani na kuipeleka kwenye magari, na kusafirisha kwenda kwenye sehemu salama.
Baada ya kazi yote, kikundi cha wanajeshi wachina wa kuokoa maafa kilifunga safari na kurudi kwenye kituo chao. Kando ya barabara ya kilomita 5, wenyeji walijaa wakiwashangilia. Wakazi hao waliwapongeza kwa shangwe na kuwashukuru wanajeshi hao wa China.
Idhaa ya Kiswahili 2005-04-08
|