Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-12 11:11:19    
Kampuni ya TCL yajulikana katika soko la dunia

cri

Miaka 23 iliyopita kijana Li Dongsheng baada ya kumaliza masoko katika chuo kikuu alirejea kwao, mji wa Huizhou mkoani Guangdong, sehemu ya pwani ya kusini mashariki ya China, na kuwa fundi wa kawaida kwenye kiwanda kimoja kidogo cha vyombo vya umeme vya nyumbani. Hivi sasa Bw. Li Dongsheng amekuwa mmoja ya wanaviwanda wanaoongoza katika sekta ya viwanda vya vyombo vya umeme nchini China, na kampuni ya TCL anayoiongoza imeendelezwa kuwa ya kwanza kwa wingi wa uzalishaji wa televisheni za rangi hapa duniani.

Bw. Li Dongsheng mwenye umri wa miaka 48, baada ya kumaliza masomo yake alianza kufanya kazi katika kiwanda kimoja cha vyombo vya umeme cha ubia kati ya China na nchi ya nje. Baadaye kiwanda hicho kikaendelezwa kuwa kiwanda kikubwa chenye pato la zaidi ya Yuan bilioni 30 kwa mwaka, ambacho hivi sasa kimekuwa kampuni inayojulikana kwa TCL yenye hisa zinazouzwa sokoni.

Bw. Li Dongsheng aliwahi kuwa fundi, msimamizi wa idara moja ya kiwanda na naibu meneja, na mwaka 1996 alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TCL kutokana na uwezo wake mkubwa wa usimamizi na teknolojia. Wakati ule kampuni za vyombo vya umeme za China zilianza kupiga hatua ya kuanzisha shughuli za uzalishaji katika nchi za nje hususan kufanya kazi za usindikaji kwa ajili ya kampuni za nchi za nje. Mwaka 1997 ulitokea mgogoro wa mambo ya fedha katika Asia ya kusini ya mashariki, ambao ulikuwa pigo kubwa kwa kampuni za vyombo vya umeme vilivyoko nchi za nje ikiwemo TCL. Tukio hilo lilimfanya Bw. Li Dongsheng kufahamu kuwa akitaka kukuza shughuli za uzalishaji katika nchi za nje, hana budi kuwa na bidhaa zenye nembo pekee ya kampuni yao.

"Mgogoro wa mambo ya fedha ya Asia ya kusini mashariki ulipunguza kwa kiwango kikubwa thamani ya fedha za nchi nyingi za sehemu hiyo isipokuwa fedha ya Renminbi ya China ilidumisha thamani yake, katika hali ya namna hiyo ni dhahiri kuwa watu wengi hawakuagiza bidhaa zao. Katika miaka miwili ya 1998 na 1999, usafirishaji wa bidhaa wa kampuni yetu ulipungua kwa mfululizo na kunisononesha sana, endapo tusingeweza kuwa na bidhaa zenye nembo yetu wenyewe, basi ingekuwa ni vigumu kwa kampuni yetu kupata maendeleo."

Baada ya kupita kwa mgogoro wa mambo ya fedha ya Asia ya kusini mashariki, Bw. Li alibuni mkakati wa maendeleo ya kampuni yao katika nchi za nje, alichagua televisheni za rangi za TCL, ambazo zilichukua nafasi bora hapa nchini, kuwa bidhaa za kundi la kwanza za kuingia kwenye soko la dunia.

Miaka mitano iliyopita kampuni ya TCL iliamua kusafirisha televisheni zake kwa nchi za Asia ya kusini mashariki ikifikiria kuwa ingawa uwezo wa uzalishaji umezidi mahitaji ya bidhaa ya sokoni, Bw. Li alifanya uchunguzi nchini Vietnam na kuona kuwa ilikuwa 45% tu ya familia za huko zilikuwa na televisheni, lakini familia nyingi zaidi za wakulima zilikuwa hazijanunua televisheni. Hivyo aliona kuwa uwezo wa masoko ya huko katika siku za baadaye bado ni mkubwa sana, licha ya hayo bei za televisheni nyingine za rangi zilizouzwa huko zilikuwa ghali na hakukuwa na huduma nzuri baada ya bidhaa kuuzwa kwa wanunuzi. Hivyo Bw. Li alitoa uungaji mkono mkubwa kwa shughuli za biashara nchini Vietnam. Kuhusu mambo hayo kiongozi mwingine wa kampuni ya TCL Bw. Yi Chunyu alisema,

"Ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 2000, watu wengi wa kampuni yetu walikuwa na maoni ya kuondoka katika soko la Vietnam, wakiona kuwa huko kuna migogoro mingi na nafasi ya maendeleo ni ndogo sana, isipokuwa wasimamizi wachache wanaoshughulikia mambo ya biashara ya nchi hiyo, mkurugenzi mkuu Bw. Li Dongsheng aliniuliza nitahitaji muda gani tena hadi kustawisha biashara ya huko, nilijibu miezi 6. Bw. Li alitangaza kuwa kuweka muda wa miezi 6 tena kwa shughuli za biashara nchini Vietnam."

Imani ya Bw. Li ilileta maendeleo, televisheni za rangi za TCL zimependwa na watu wengi wa Vietnam, ambapo kampuni ya TCL iliahidi kuwa televisheni za TCL zinashughulikiwa bila malipo yoyote kwa muda wa miaka mitatu.

Kwa kufuata, Bw. Li Dongsheng akasafirisha televisheni za rangi za TCL katika masoko ya nchi nyingi za Asia ya kusini mashariki, baada ya hapo alizisafirisha hadi kwenye masoko ya Ulaya na Marekani.

Mafanikio waliyopata yameimarisha imani ya Bw. Li Dongsheng ya kuingia kwenye soko la dunia. Mwezi Agosti mwaka 2004, kampuni ya TCL ilitenga dola za kimarekani milioni 130 kununua kampuni ya mashuhuri ya televisheni Thomson Electronics Limited nchini Ufaransa na kuanzisha kampuni ya TCL- Thomson Electronics Limited nchini humo. Hadi hapo, kampuni ya TCL ilikuwa na vituo vitano vya utafiti, viwanda 10 za uzalishaji na vituo vya mauzo ya seti zaidi ya elfu 20 duniani. Mwaka 2004, kampuni ya TCL iliuza televisheni za rangi zaidi ya milioni 17 duniani ikiwa ni ongezeko la karibu 50% kuliko mwaka uliotangulia. Mwaka ule ule kampuni TCL ilinunua kampuni ya simu za mikononi ya Alcatel Mobile Phones Limited na kuanzisha kampuni mpya ya TCL-Alcatel ambayo ni ya 7 kwa ukubwa wa uzalishaji wa simu za mikononi duniani.

"Napongeza sana uamuzi wa mkurugenzi mkuu Li, ambao umeunganisha utaratibu na utamaduni wa nchi mbili, huu ni msingi wa kupata mafanikio mapya."

Bw. Li alisema kuwa kampuni ya TCL inanuia kuwa na pato la Yuan bilioni 70 mwaka huu na kuwa na pato la Yuan bilioni 150 ifikapo mwaka 2010. Kampuni ya TCL itakuwa ya kimataifa na kuwa na nguvu ya ushindani katika soko la dunia.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-12