Mahitaji
Nyama ya kondoo gramu 500, karoti moja, mchele, vitunguu, chumvi na mafuta
Njia
1. Osha mchele, karoti na nyama ya kondoo. Kata karoti na vitunguu viwe vipande vipande. Loweka mchele kwa maji yenye chumvi kwa dakika 15.
2. Tia mafuta ndani ya sufuria na chemsha mpaka iwe na nyuzi 50, tia vipande vya vitunguu halafu tia vipande vya nyama ya kondoo, tia chumvi kidogo, korogakoroga kwa dakika 10, kisha vipakue.
3. tia mafuta tena ndani ya sufuria, tia mchele na karoti na tia vipande vya nyama kwenye michele, mimina maji kidogo, baada ya kuchemka punguza moto kidogo na endelee kuchemsha kwa dakika 20. Mpaka hapo pilau hiyo iko tayari kuliwa.
|