Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-15 10:13:53    
Ndugu Zhou Qiang na harakati za kulinda mito Mama

cri

Harakati za kulinda Mto Mama zilianzishwa mwaka 1999, madhumuni yake ni kulinda mazingira ya Mto Manjano na Mto Changjiang ya China.

Harakati za kulinda Mto Mama ilianzishwa na Umoja wa vijana wa China, Kamati ya kupanda miti ya China, Kamati ya hifadhi ya mazingira na mali asili ya bunge la umma la taifa, kamati ya mazingira, mali asili na watu ya baraza la mashauriano ya kisiasa, wizara ya hifadhi ya maji, wizara ya kilimo, Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China na wizara ya misitu.

Harakati za kulinda mito Mama ina kazi 4 muhimu: kwanza?kutunza na kuenzi utamaduni wa hifadhi ya mazingira ya asili, kuwaelimisha watoto na vijana umuhimu wa maji, kuzidisha ufahamu wao wa kulinda Mto Mama na uwiano wa maendeleo ya binadamu na mazingira. Pili, kuwawezesha watoto na vijana kutambua hali halisi ya mito Mama na kuwaandaa wawe na desturi nzuri za kuhifadhi mazingira tangu utotoni. Tatu, kuanzisha miradi ya vielelezo vya hifadhi ya mazingira ya asili, kuweka mkazo katika kuchagisha fedha kwa ujenzi wa miradi ya vielelezo ili kuboresha moja kwa moja mazingira ya asili ya mito mikubwa. Nne, kufanya mawasiliano na ushirikiano na vijana wa nchi nyingine katika sekta ya hifadhi ya mazingira, ili kuwawezesha watoto na vijana wa nchi mbalimbali kufanya mazungumzo, kufundishana, kuzidisha urafiki na kulinda mito Mama kwa pamoja.

Mkuu wa kikundi cha uongozi cha harakati za kulinda mito Mama Bw. Zhou Qiang alitoa sera nyingi kubwa kuhusu hifadhi ya mito mama, na kushiriki shughuli na miradi mbalimbali mikubwa kuhusu hifadhi ya mazingira. Harakati za kulinda mito Mama zilichukua hatua ya " kupanda mti mmoja kwa Yuan 5, kupanda miti ya Hekta 1/15 kwa Yuan 200". kwa kutumia njia hii, washiriki wa harakati hizo walichangisha fedha za jamii kwa Yuan milioni 210, na vijana wengi zaidi walihudhuria harakati za kulinda mito Mama, na kusukuma juhudi za hifadhi ya mazingira ya China.

Tangu kuanzishwa kwa harakati za kulinda mito Mama, katika miaka 6 iliyopita, miradi 1103 ya kupanda miti imekamilishwa, maeneo ya miradi hiyo yalifikia Hekta laki 2.66; vijana milioni 300 walishiriki kwenye shughuli za kupanda miti ili kulinda mito Mama; kufanya maingiliano na ushirikiano na vijana wengine wa nchi 30, na kuleta athari kubwa nchini China na dunia.

Shirikisho la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa, ukiwa jumuia ya kitaifa, Umoja wa vijana wa China imekuwa nguvu kubwa katika hifadhi ya mazingira ya China na dunia.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-15