Naibu waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya Kusini jana alisema kuwa, bara la Afrika ambalo liko nyuma kabisa kiuchumi duniani linataka kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati na bara la Asia ambalo uchumi wake unaendelea haraka, ili kubadilishana uzoefu wa maendeleo na kujenga kwa pamoja siku za usoni zenye wenye utulivu na ustawi.
Alisema kuwa, Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini pamoja na viongozi wa nchi zaidi ya 50 za Asia na Afrika watahudhuria mkutano wa pili wa Asia na Afrika utakaofanyika huko Djakarta kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 23 mwezi huu, na kujadiliana kuhusu kuimarisha ushirikiano katika fani mbalimbali kati ya mabara hayo mawili.
Mwaka jana, wawakilishi wa nchi husika walifanya mkutano nchini Afrika ya Kusini, kutoa miradi halisi ya ushirikiano kati ya Asia na Afrika, hasa ushirikiano wa kiuchumi na mawasiliano ya kiutamadani, na kuweka msingi kwa pande hizo mbili kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati. Mkutano huo utakaofanyika utatoa fursa nzuri kwa viongozi wa nchi za mabara hayo mawili kubadilishana uzoefu, kupanua maoni ya pamoja na kuanzisha ushirikiano.
Habazi zinasema kuwa, baada ya kuanzishwa kwa uhusiano huo, nchi za Asia na Afrika zitashirikiana, kubadilishana na kufundishana maarifa ya maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, kuweka mpango halisi ili kutimiza lengo la kujenga Asia na Afrika zenye amani, utulivu, maendeleo na ustawi zaidi.
Mkutano wa kwanza wa viongozi wa nchi za Asia na Afrika ulifanyika huko Bandong, Indoneisa mwezi Aprili mwaka 1955. kwenye mkutano wa 8 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki uliofanyika huko Phnom-penh mwezi Novemba mwaka 2002, Rais Mbeki wa Afrika ya Kusini aliyehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Umoja wa Afrika, alitoa pendekezo kwa mara ya kwanza kuunda upya mfumo wa ushirikiano wa Asia na Afrika, na kuimarisha ushirikiano huo. Rais wa wakati huo wa Indonesia Bi. Megawati aliitikia pendekezo hilo, na baadaye Afrika na Kusini na Indonesia zilifanya kwa pamoja mikutano miwili ya kikanda ya mawaziri na kazi katika mwaka 2003 na mwaka 2004, ili kuandaa mkutano huo wa wakuu wa nchi za Asia na Afrika.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-15
|