Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-15 20:43:08    
Jumba la Muziki la Beijing

cri

Jumba la Muziki la Beijing, ambalo ni la hali ya juu kabisa nchini China kwa kutumbuiza muziki pekee, linajulikana sana kwa maonesho ya upigaji wa muziki hali ya juu. Ndani ya jumba hilo kuna mapambano ya anasa na mwangaza mwanana wa taa zinazomulika kutoka pande zote nne. Kwenye kuta za ukumbi wa mapumziko na kwenye ujia, kumetundikwa picha za wanamuziki mashuhuri. Tangu jumba hilo lilipofunguliwa mwaka 1985, baadhi ya wakati lilikuwa likistawi, na wakati mwingine huko hapa kusikiliza muziki.

Siku ya Mwaka Mpya ya 1995, Thieta kuu ya Opera ilionyesha tamasha la muziki hapo. Gazeti moja liliandika hivi: "Kengele ya Mwaka Mpya ilipigwa katika maonesho ya michezo ya sanaa. Tamasha la muziki lilianzishwa na nchi za Magharibi, China iliiga kwa mafanikio, na Kituo cha Televisheni cha Taifa kilitangaza tamasha hilo. Mwaka huu, Jumba la Muziki la Beijing lilipiga hatua kubwa, magazeti na televisheni vinatangaza habari zake nyingi.

Ili kufanya watazamaji wengi zaidi wapate nafasi ya kusikiliza muziki wa hadhi ya juu, mwezi Februari, Jumba la Muziki la Beijing liliyatangulia majumba mengine kuchukua hatua ya "kutazama mazoezi", yaani watazamaji walinunua tikiti za mchana na kutazama mazoezi ya wanamuziki. Katika siku ya kwanza, tikiti 500 ziliuzwa kwa mkumbo mmoja. Kwa mashabiki wa muziki, hatua hiyo bila shaka ni jambo zuri lililowafurahisha.

Tarehe 2 Aprili, Bw. Jiang Zemin, Rais wa zamani wa China alifika Jumba la Muziki la Beijing kuhudhuria tamasha la muziki la maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa mwanamuziki mzalendo Liu Tianhu.

Tarehe 31 Mei, Jumba la Muziki la Beijing lilifanya tumbuizo la pili ili kuchangisha fedha za kuwasaidia watoto 100 walioachishwa masomo kutokana na kukosa ada. Mchango wa yuan laki moja ulitumiwa kwa kujenga shule ya msingi ya tumaini huko wilaya ya Jingle, mkoani Shanxi.

Kuanzia mwezi Agosti hadi Novemba, matamasha manane ya muziki yalifanyika kwenye Jumba hilo la Muziki la Beijing, ambapo benki ya "ensemble"na benki ya "chamber" zilishirikiana katika maonesho. Mchanganyiko huu ni uvumbuzi, ulipongezwa sana na wasikilizaji.

Mwishoni mwa mwaka 1995, taa za rangi zilikuwa zinametameta kwenye miti ya Kristmas ndani ya Jumba la Muziki la Beijing. Matamasha ya muziki ya mwaka mpya yalifanyika kwa shamrashamra. Matamasha hayo yalifanywa na vikundi 6 vya muziki tangu tarehe 24 Desemba, na wakati wa kila tamasha jumba lilijaa watazamaji, hata jumba hilo ilibidi kuuza tikiti za kusimama. Mwanzoni mwa mwaka 1996, ili kuridhisha maombi ya watazamaji, jumba hilo liliongeza matamasha 7 ya kiwango cha juu.

Kutokana na ufanisi wa Jumba la Muziki la Beijing, si vigumu kwa watu kuelewa kuwa katika miaka ya karibuni, wananchi wengi zaidi wanapenda kuburudika kwa muziki wa kiwango cha juu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-15