Tarehe 15, Mwezi Machi, mwaka 2005, Shirikisho la Afrika na Sehemu ya Mashariki ya kati la biashara na China na Shirikisho la wafanyabaishara wa viatu la Huizhou mkoani Guangdong yalisaini makubaliano kuhusu "Mradi wa bilioni 10". Kutokana na makubaliano hayo, Shirikisho la Afrika na sehem ya Mashariki ya kati la biashara na China litatoa misaada mbalimbali kwa mashirika ya viatu ya Huidong ili kuyasaidia kuanzisha shughuli katika bara la Afrika, sehemu ya mashariki ya kati na Umoja wa Ulaya, pia kuyasaidia kuongeza mapato hadi kufikia yuan za renminbi bilioni 10.
Naibu mkuu wa Shirikisho l wafanyabiashara wa viatu la Huizho Bwana Ou Jiyang alisema kuwa, Mradi wa bilioni 10 unalenga kuhimiza mashirika ya viatu ya Huidong kuingia kwenye masoko ya Afrika, sehemu ya mashariki ya kati na Umoja wa Ulaya kupitia Shirikisho l Afrika na sehemu ya mashariki ya kati la biashara na China, ili kufanya shughuli za biashara kwa muda mrefu katika sehemu hizo. Shirikisho hilo litatoa misaada halisi ya miaka miwili kwa mashirika ya viatu ya Huidong. Lengo la mwaka wa kwanza ni kuyasaidia kuongeza mapato kuwa yuan za renminbi milioni 200 kutoka milioni 100, na lengo la mwaka wa pili ni kuongeza mapato kuwa milioni 500 kutoka milioni 300. Kutokana na msingi huo, Shirikisho la Afrika na sehemu ya Mashariki ya kati la biashara na China litayasaidia mashirika ya viatu ya Huidong kuongeza mapato hadi kufikia yuan za renminbin bilioni 10.
Bwana Ou Jiyang alieleza kuwa, tangu wafanyabiashara wa Hongkong waanzishe kiwanda cha kwanza cha viatu katika Wilaya ya Huidong mkoani Guangdong mwaka 1982, wilaya hiyo imekuwa na mawasiliano barabara na kampuni za Hongkong. Hivi sasa , wilaya hiyo imekuwa kituo kikubwa zaidi cha kutengeneza viatu vya wanawake vyenye mitindo ya kisasa, na kuna jumla ya mashirika zaidi ya 3000, na thamani ya jumla ya uzalishaji wa mashirika hayo ilifikia yuan bilioni 10, na viatu vinavyouzwa kwenye sehemu mbalimbali nchini na kusafirishwa katika nchi za nje ni nusu kwa nusu.
Bwana Ou Jiyang alisisitiza kuwa, ingawa viatu vya Huidong vinasafriishwa katika nchi mbalimbali duniani zikiwemo Marekani na nchi za Ulaya, lakini faida zake siyo kubwa. Baada ya kushirikiana na Shirikisho la Afrika na sehemu ya mashariki ya kati la biashara na China, Shirikisho la wafanyabiashara wa viatu la Huidong linaweza kuongeza mauzo yake, na kuanzisha njia ya kudumu ya biashara, kutengeneza bidhaa zake zenyewe, na kuwawezesha wateja na mashirika kuwasiliana moja kwa moja. Njia hizo zinasaidia kuongeza ufanisi wa mashirika, pia zinasaidia kuenzi sifa ya bidhaa za mashirika ya viatu ya Huidong duniani.
Bwana Ou Jiyang alieleza kuwa, kutokana na misaada kwa mashirika ya viatu ya Huidong, Shirikisho la Afrika na sehemu ya mashariki ya kati la biashara na China limepata faida, wafanyabiashara wengi wa shirikisho hilo wamepata fursa za kiabiashara, ushirikiano kati yao na mashirika ya Huidong ya mkoa wa Guangdong, China unanufaisha pande hizo mbili.
Meneja mkuu wa Shirikisho la Afrika na sehemu ya mashariki ya kati la biashara na China Bwana Shen Bozhao alisema kuwa, shirikisho hilo litafanya ukaguzi huko Huidong ili kuzidisha ushirikiano na mashirika ya viatua ya Huidong.
Bwana Shen Baozhao alisema kuwa, ana imani kubwa juu ya "Mradi wa bilioni 10". Katika miaka mitatu iliyopita tangu Shirikisho la Afrika na sehemu ya Mashariki ya kati la biashara na China kuanzisha ushirikiano wake na China, shirikisho hilo limesaidia usafirishaji wa bidhaa za vyombo vya umme vya China kwenda kwenye soko la Afrika na sehemu ya mashariki ya kati, sasa viatu vya mashirika ya Huidong vinakaribishwa sana kwenye masoko ya barani Afrika na sehemu ya mashariki ya kati.
Bwana Ou Jiyang alisema kuwa, viatu vya Huidong viliingia kwenye masoko makubwa matatu kupitia Shirikisho la la Afrika na sehemu ya mashariki ya kati la biashara na China, na viatu vya aina mbalimbali vinauzwa kutokana na mahitaji tofauti ya sehemu mbaimbali, hivyo biashara inayasaidia sana maendeleo ya mashirika viatu vya Huidong.
Shirika la viatu la Yuanfeng la Huizhou alimwambia mwandishi wa habari kuwa, zamani bidhaa za shirika hilo zilisafirishwa katika nchi za mashariki ya kati, lakini ilikuwa ni vigumu kuendeleza shughuli peke yake katika nchi hizo. Hivi sasa shughuli zinaendelea katika hali ya ushirikiano kati ya mashirika ya China na shirikisho la nje, anafurahia sana.
Idhaa ya Kiswahili 2005-04-15
|