Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-21 21:10:34    
Sekta ya uzalishaji wa Chakula ya China

cri

Baada ya maendeleo ya miaka zaidi ya 50, shughuli za uzalishaji wa chakula nchini China zimebadili hali ya zamani ambayo zilikuwa na uzalishaji wa chakula wa aina chache tu. Kwenye msingi wa kupanua uzalishaji wa aina za zamani, aina nyingi mpya za uzalishaji wa chakula zimeanzishwa na kupata maendeleo makubwa.

Mwaka 1993, kituo cha maendeleo ya chakula kisicho na uchafuzi cha China kilishiriki kwenye Shirikisho la harakati za kilimo mahuluku la kimataifa (IFOAM). Na hivi sasa kimeanzisha uhusiano na nchi na sehemu zaidi ya 90 na mashirika zaidi ya 500 duniani, na kuanzisha mawasiliano na ushirikiano nao katika vigezo vya sifa za bidhaa na teknolojia za kutengeneza bidhaa, usimamizi wa idhini na kanuni za biashara. Si kama tu kimeongeza umaarufu wa chakula kisicho cha uchafuzi cha China duniani na kuinua sifa yake, bali pia iliifanya thamani ya biashara ya chakula cha China katika nchi za nje iongezeke maradufu kila mwaka katika kipindi cha mwaka 1997 hadi mwaka 1999. Mkoa uliouza chakula kingi zaidi katika nchi za nje ni mkoa wa Shandong, ambao uliuza chakula tani elfu 680. Aina muhimu za chakula hizo ni maharagwe, matunda na mboge, na thamani ya mauzo ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 45.

China ina historia zaidi ya miaka 5000 ya maendeleo ya kilimo, na ina desturi ya kutotumia mbolea za kikemikali na dawa za kikemikali mashambani. Nguvu kazi nchini China ni nyingi, na uzalishaji wa chakula kisicho na uchafuzi ndio ni uzalishaji unaohitaji nguvu kazi nyingi. Uzoefu wa uzalishaji katika miaka kumi iliyopita umethibitisha kuwa, asilimia 90 ya mashirika yamepata faida nyingi baada ya kuzalisha chakula kisicho na uchafuzi.

Kutokana na ongezeko la athari ya mauzo ya chakula kisicho na uchafuzi ya China katika nchi za nje, chakula cha aina hiyo cha China kinafuatiliwa sana na nchi za nje. Kampuni nyingi za Marekani, Japan, Ujerumani zinataka kununua chakula kisicho na uchafuzi kutoka China.

Ili kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya chakula, serikali ya China itachukua hatua husika. Kwanza, serikali itaendelea kutunga sera za kuyanufaisha mashirika husika, na kuanzisha mashirika ya kielelezo ya kuzalisha chakula katika sehemu zinazozalisha mazao na zenye kiwango cha juu cha teknolojia. Aidha, serikali itatunga mpango wa ujumla kuhusu sekta ya uzalishaji wa chakula ili kuisimamia kwa ujumla. Pili, serikali itarekebisha mfumo wa sekta hiyo kwenye msingi wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, kusukuma mbele maendeleo ya sekta nzima kwa kuinua kiwango cha uzalishaji wa aina kadhaa kwanza, na kuyahimiza mashirika makubwa ya uzalishaji wa chakula kujenga idara za utafiti wa sayansi na teknolojia. Tatu, China itajenga mfumo kamili wa uhakikisho wa sifa za bidhaa. Katika kipindi cha mpango wa 10 wa maendeleo ya miaka mitano, China itaimarisha usimamizi wa usalama wa chakula na kusimamia sifa za chakula kwa njia ya kutunga sheria na kuanzisha mfumo mzuri wa usimamzi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-21