Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-26 16:51:43    
Kutulia kwa kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni na fedha ya China kuna manufaa kwa dunia

cri
Jumuiya ya kimataifa inafuatilia mara kwa mara suala la kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa fedha za kichina, tangu China ilipoanza kutekeleza sera kuhusu kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa fedha ya Renminbi miaka zaidi ya kumi iliyopita. Hivi karibuni kuongezwa kwa thamani ya fedha ya Renminbi au la, kumekuwa tena moja ya masuala yanayofuatiliwa sana na watu. Kuhusu suala hilo, mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alikuwa na mahojiano na baadhi wa wataalamu wa uchumi wa China na wa nchi za kigeni ambao walisema kuwa, kutulia kwa kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa fedha za Renminbi kunanufaisha maendeleo ya uchumi wa China na dunia. Wataalamu hao wa uchumi pia wanasifu jitihada za serikali ya China katika kuboresha utaratibu wa kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni.

Tangu mwaka 1994 China imekuwa ikitekeleza sera moja ya usimamizi wa kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni, ambacho kinaamuliwa na hali halisi ya ununuzi na uuzaji wa sokoni na kufuatilia moja kwa moja dola ya kimarekani, ambapo benki kuu ya China inatangaza kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni kwa mujibu wa hali halisi ya soko la sarafu duniani. Tangu kuanza kutekelezwa kwa sera hiyo, kiasi cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni kwa ujumla kimetulia. Wataalamu wanasema kuwa sera hiyo ya ubadilishaji wa fedha imekuwa ikitulia tangu ianze kutekelezwa.

Katika miaka ya karibuni pato kutokana na biashara ya China na nchi za nje lilichukua nafasi kubwa mwaka hadi mwaka katika jumla ya pato la China, na lilifikia dola za kimarekani trilioni 1.15, ambayo ilichukuwa nafasi ya tatu duniani. Katika muda huo uwekezaji wa nchi za nje nchini China uliongezeka mwaka hadi mwaka, na ulifikia dola za kimarekani bilioni 60 kwa mwaka 2004 ukichukua nafasi ya pili duniani. Bw. Zhao Xijun kutoka taasisi ya utafiti wa mambo ya fedha na hisa za kampuni ya Chuo kikuu cha Umma cha China anaona kuwa biashara ya nje na uwekezaji wa nchi za kigeni ni muhimu sana kwa nchi zinazoendelea kama China, na mafanikio iliyopata China katika miaka ya karibuni katika upande huo yanahusiana kwa kiasi fulani na kutulia kwa kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni. Alisema,

"Sababu moja muhimu kwa China kupata maendeleo makubwa katika biashara ya nje ni sera tulivu za kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni, kampuni na viwanda vilivyofanya biashara na nchi za nje havikuwa na wasiwasi kuhusu mgogoro unaoletwa na mabadiliko makubwa ya kiasi cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni. Kwa mfano endapo thamani ya Renminbi inaongezeka kwa ghafla, italeta mabadiliko mengi yakiwa ni pamoja na kupungua kwa uzalishaji wa viwanda vinavyojihusisha na biashara ya nje. Hivi sasa sera tulivu kuhusu kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni, pia ni dhamana kwa imani ya wawekezaji nchini China. Endapo kiwango hicho kinabadilika mara kwa mara, kitaongeza gharama na hatari ya uwekezaji, hivyo kiwango tulivu cha kubadilisha fedha kinavutia zaidi wawekezaji. Bw. Zhao alisema,

"Marekani inachukua nafasi ya kwanza duniani katika mambo ya biashara ikifuatiwa na Japan, eneo la nchi za Umoja wa Ulaya zinazotumia Euro pamoja na China. Uchumi wa dunia ukitaka kuwa na maendeleo ya utulivu, basi unahitaji mazingira ya utulivu ukiwemo uhusiano tulivu wa pande hizo nne muhimu za kiuchumi, endapo thamani za fedha zinabadilika mara kwa mara, ni dhahiri kuwa hakunufaishi maendeleo ya biashara ya kimataifa, bali kinyume chake kutaongeza mgogoro na gharama za biashara ya kimataifa.

Katika miaka ya karibuni baadhi ya nchi zinaishinikiza serikali ya China mara nyingi iongeze thamani ya fedha ya Renminbi. Kuhusu hali hiyo profesa Robert A. Mundell ambaye ni mwanzilishi wa Euro anaona kuwa, kutulia kwa kiasi cha kubadilisha fedha ya Renminbi na fedha za kigeni kutafanya kazi muhimu ya kuhimiza maendeleo ya utulivu ya uchumi wa dunia. Anaona kuwa baadhi ya nchi zilizoendelea, ambazo hazina ongezeko kubwa la uchumi, zinadai kuwa Renminbi inatakiwa kuongezeka thamani yake kutokana na matakwa ya kisiasa. Hivi sasa Renminbi inatakiwa kudumisha utulivu. Alisema,

"Kuongezeka kwa thamani ya Renminbi kutapunguza idadi ya wawekezaji kutoka nchi za nje, na kuongeza mchakato wa kufanya Renminbi kuwa moja ya fedha zinazokubalika duniani. Kiuchumi, kudai Renminbi iongezeke thamani yake siyo hoja ya haki, bali ni baadhi ya watu wanafikiria zaidi kisiasa. Kufanya hivyo kutaleta hali isiyo ya utulivu katika sehemu ya Asia ya kusini mashariki, hata kutaiathiri China kutekeleza ahadi ilizotoa wakati ilipojiunga na WTO."

Serikali ya China imesema mara nyingi kuwa katika siku za baadaye itachukua hatua nyingi kuboresha na kufanya mageuzi kuhusu utaratibu wa kiwango cha kubadilisha Renminbi na fedha za kigeni.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-26