Yixing ni mji mdogo wa mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. Mji huo unaegemea milima na Ziwa Taihu inayojulikana, mandhari yake inapendeza sana. Mbali na mandhari yake nzuri, mji Yixing pia una vivutio vingi vya kiutamaduni. Watu wengi waliowahi kufanya utalii mjini Yixing hawakujisikia uchovu na waling'ang'ania huko.
Mji Yixing ulikuwa na historia ndefu na utamaduni unaong'ara ambao uliacha mali nyingi za urithi mjini humo. Mabaki ya kale maarufu kama vile Mnara wa mawe wa Guoshan wa zama za madola matatu ya karne ya kwanza; Tanuri la Gulong la Enzi ya Tang ya karne ya 7; na Jumba la vitabu la Dongpo lililojengwa kumkumbuka mwandishi maarufu wa Enzi ya Song ya kaskazini Su Dongpo. Zaidi ya hayo, katika zama za vyombo vipya vya mawe miaka zaidi ya 5000 iliyopita, wakulima wa sehemu hiyo walivumbua vyombo vya ufinyanzi. Baadaye vyombo vya ufinyanzi vya Yixing vinajulikana nchini China, miongoni mwa vyombo hivyo, ustadi wa ufinyanzi wa vyombo vya udongo mwekundu mweusi ni maarufu zaidi, udongo huo wa kufinyanga vyombo ni laini sana, vyombo vilivyofinyangwa kwa udongo huo pamoja na mapambo ya kiasili vinapendeza sana. Bwana Nie Zhongyuan aliyewahi kwenda Yixing mara kadhaa anaupenda sana mji huo mdogo, alisema:
Mji huo mdogo una mandhari nzuri ya kimaumbile pia una vivutio vya kiutamaduni. Milima, maji ya ziwa na mawe ya mji huo vinajulikana nchini na ng'ambo. Mbali na vyombo vya ufinyanzi, maandiko ya kichina na uchoraji wa picha wa mji huo pia vinawavuta sana watu.
Ni kweli kama alivyosema, wachoraji wengi maarufu kama vile Xu Beihong, Wu Dayu, Yin Shoushi na Wu Guanzhong, , walizaliwa katika mji huo mdogo. Wasanii hao wameacha sanaa mbalimbali zinazong'ara sana nchini. Katika mji Yixing wa hivi sasa, wachoraji picha wa kizazi kipya pia wanajitahidi sana katika kazi zao. Katika mitaa hata vichochoro vya mji wa Yixing, watu wanaweza kuona maonesho ya aina mbalimbali ya maandiko ya kichina na picha zilizochorwa, hivyo vimekuwa vivutio pekee vya mji huo mdogo. Bwana Nie alisema:
Jumba la sanaa ya uchoraji la Yixing limewashirikisha wachoraji wa sehemu mbalimbali nchini China, hivyo kila mara linaweza kufanya maonesho ya maandiko ya kichina na picha zilizochorwa, maonesho hayo yanavutia sana watalii waliotembelea mji huo.
Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, serikali ya mji wa Yixing ilitenga fedha kujenga Jumba la kumbukumbu Xu Beihong, Jumba la sanaa la Yixing pamoja na Jumba la sanaa ya Yin Shoushi, Jumba la vyombo vya ufinyanzi na kadhalika, mjini humo pia kuna mashirikisho mbalimbali ya maandiko ya kichina na uchoraji wa picha, hivyo shughuli za kiutamaduni mjini Yixing zimesitawi sana.
Mbali na mabaki mengi ya kale, kutokana na sura ya ardhi ya chokaa, mjini Yixing kuna mapango mengi yenye maumbile ya ajabu, na mapango hayo mengi yanahusiana na wasomi na wachoraji. Miongoni mwa mapango hayo, pango la Shanjuan lililofunguliwa mwaka 1934 liliumbika kwa miaka milioni moja. Jina lake Shanjuan lilitokana na mtawa mmoja aitwaye Shanjuan ambaye aliishi ndani ya pango hilo kabla ya miaka 4000 na kitu. Pango hilo liko umbali wa kilomita 25 kutoka mji Yixing. Hivi sasa pango hilo limekuwa bustani na sehemu yenye vivutio vingi kwa watalii.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-09
|