Mfumuko wa bei ya nyumba za makazi umekuwa moja ya suala nyeti linalofuatiliwa na watu wa sekta mbalimbali ya jamii hapa nchini. Wataalamu husika wamesema kuwa mfumuko wa bei ya nyumba za makazi pamoja na vitendo vya kutaka kujipatia faida kubwa kwa kutumia nafasi hiyo ya biashara Speculate, huenda vitasababisha kuanguka kwa biashara ya nyumba za makazi na mgogoro wa mambo ya fedha tena vitaathiri vibaya maendeelo mwafaka endelevu ya uchumi wa China. Ili kuzuia kutokea kwa hali ya namna hiyo, hivi sasa serikali ya China imetoa sera mpya kuhusu mambo ya fedha, kodi na ardhi ili kuzuia mfumuko wa bei ya nyumba za makazi na hali ya kushamiri kupita kiasi ya biashara hiyo.
Katika miaka ya karibuni suala lililofuatiliwa zaidi katika soko la nyumba za makazi lilikuwa ni mfumuko wa bei yake. Takwimu inaonesha kuwa wastani wa bei ya nyumba za makazi uliongezeka kwa zaidi ya 14% mwaka 2004 kuliko mwaka uliotangulia, ambao umekuwa mwaka wenye kupanda kwa kiasi kikubwa zaidi kwa bei ya nyumba za makazi kwa kipindi cha miaka 7 iliyoptia. Baada ya kuingia mwaka 2005, hali ya kupanda kwa bei ya nyumba za makazi haikupungua kwa udhahiri. Takwimu iliyotolewa hivi karibuni na idara ya takimu ya taifa inaonesha kuwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu bei ya nyumba za makazi ilipanda kwa kiasi cha 10% katika miji 35 mikubwa na wastani, na katika baadhi ya miji bei hiyo ilipanda hata kukaribia 20%, ambapo wakazi wa kawaida wameshindwa kununua nyumba kwa uwezo wao.
Naibu kiongozi wa idara ya utafiti wa mambo ya fedha na vyeti vya hisa ya Chuo Kikuu cha Wananchi profesa Zhao Xijun, ambaye amefanya utafiti tangu miaka mingi iliyopita kuhusu soko na nyumba za makazi, anaona kuwa mfumuko wa bei ya nyumba za makazi nchini ulisababishwa na mambo mengi.
"Utatuzi wa suala la nyumba za makazi kwa wananchi wa China bado uko mbali sana, nyumba walizonunua kwa 80% ya wanunuzi zilikuwa ni za makazi kwa wao wenywe. Hivi sasa China iko katika kipindi chenye ongezeko la kasi la uchumi, katika kipindi kilichopita tulijitahidi kutatua tatizo la njaa likiwa ni pamoja na chakula na nguo, nyumba na mawasiliano vitakuwa suala muhimu litakalotatuliwa katika siku za baadaye, hususan nyumba ya makazi, watu wengi wanataka kuboresha mazingira yao ya makazi, hivyo yatatokea mahitaji makubwa ya nyumba za makazi. Mahitaji hayo hayawezi kutatuliwa katika miaka michache, hali ambayo inafanya bei ya nyumba za makazi kuendelea kupanda katika miaka mingi ijayo."
Soko motomoto la nyumba za makazi si kama tu linavutia macho ya wakazi wanaotarajia kuboresha mazingira yao ya kukaa, bali pia limekuwa sekta inayowavutia zaidi wawekezaji. Kutokana na kuwa hivi sasa nafasi ya uwekezaji bado ni ndogo, hivyo si rahisi kwa kampuni na wakazi wenye fedha nyingi kupata njia nzuri ya uwekezaji, kwa hiyo wakatupia macho soko la nyumba za makazi, ambalo ni rahisi kupata faida kubwa. Bw. Song Peng ni mmoja wa watu wa aina hiyo, mwandishi wetu wa habari hivi karibuni katika maonesho ya biashara ya nyumba za makazi yaliyofanyika mjini Nanjing alimwona bwana huyo, ambaye alikuwa akitaka kununua nyumba moja ya uwekezaji. Alimwambia mwandishi wetu wa habari,
"Nyumba hiyo ninayonunua ni kwa ajili ya uwekezaji wala siyo kwa ajili ya kukaa, ninaona kuwa hivi sasa watu wengi wanawekeza katika sekta za nyumba na makazi, na kwa hivi sasa mimi sina matumizi na fedha nilizo nazo."
China kuna watu wengi wenye mawazo kama ya bwana Song, kuna baadhi ya watu ambao hata wamenunua nyumba miongo kadhaa kwa ajili ya uwekezaji, na katika baadhi ya sehemu yameanzishwa makundi maalumu yanayoshughulikia uwekezaji wa nyumba za makazi. Wataalamu wanasema kuwa kuwepo uwekezaji mwingi katika sekta ya nyumba za makazi ni chanzo kingine kilichosababisha mfumuko wa bei ya nyumba za makazi. Vitendo hivyo vya uwekezaji vimesababisha kupanda kwa bei ya nyumba za makazi na kuhamasisha uwekezaji katika sekta za chuma na chuma cha pua, saruji na nyinginezo, jambo ambalo limezidisha hali ya shida ya nishati, vifaa na mali-ghafi pamoja na mawasiliano.
Mufumuko wa bei ya nyumba za makazi pamoja na "hatari ya mapovu" na athari mbaya zitakazoweza kutokea katika baadhi ya miji ya China imezingatiwa na serikali. Hivi sasa serikali ya China imeamua kuchukulia udhibiti wa bei ya nyumba za makazi kuwa moja ya mambo ya mpango wa udhibiti wa uchumi wa taifa.
Hatua ya kwanza iliyochukuliwa dhidi ya mfumuko wa bei ya nyumba za makazi ni kuongeza riba ya mikopo ya nyumba. Profesa Yi Zhongli wa taasisi ya sayansi ya jamii ya China alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,
"Hii ni hatua ya kwanza, ambayo lengo lake ni kudhibiti mfumuko wa bei za nyumba za makazi tu."
Wataalamu wa uchumi wanaona kuwa pamoja na utekelezaji wa sera za udhibiti wa mfumuko wa bei za nyumba, kasi hiyo itapungua.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-10
|