Mji wa Shenzhen ni mji wa pwani ulioko kusini mwa china. Uko katika kusini ya mstari wa tropiki ya Kansa. Kwa upande wa mashariki unapakana na Ghuba ya Daya na Ghuba ya Dapeng, kwa upande wa magharibi inakaribia sehemu ya mwisho ya Mto Zhujiang na bahari ya Lingding, kwa upande wa kusini unaunganishwa na Hongkong na Mto Shenzhen, na kwa upande wa kaskazini unapakana na miji ya Dongguan na Huizhou.
Hali ya hewa huko Shenzhen ni ya aina ya bahari ya ukanda wa nusu-tropiki, ambayo ni ya fufutende, yenye mvua za kutosha na mwanga wa jua wa kutosha. Joto la wastani la mwaka mzima ni nyuzi 23.7 sentigredi. Kipindi kutoka mwezi Mei hadi mwei Septemba kila mwaka ni masika. Kiasi cha wastani cha mvua kwa mwaka ni milimita 1608.1. Tufani chache zinatokea katika majira ya joto na ya Autumn.
Eneo la mji wa Shenzhen ni kilomita za mraba 1952.84. Miongoni mwa eneo hilo, eneo maalum ya kiuchumi ni kilomita za mraba 359.81.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003, eneo la ardhi zinazoweza kutumika kwa ujenzi mjini humo zilikuwa ni kilomita za mraba 931, ambalo linachukua asilimia 46.1 ya eneo lote la mji huo. Na eneo la kilomita za mraba 488 limetumiwa.
Mwaka 1979, mapato ya uzalishaji nchini (GNP) kwa kila mtu ni yuan za renminbi 606 tu, hadi mwaka 2003, mapato hayo yalifikia yuan 54,545, sawa na dola za kimarekani 6590.
Katika muda mrefu bidhaa za chakula wakiwemo ndege, mayai, samaki nyama, mboga na nyama katika soko la Hongkong zinaagizwa kutoka Shenzhen. Kila mwaka bwawa la Shenzhen linapeleka maji mita za ujazo zaidi ya bilioni 1.1 huko Hongkong, na kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha Dayawan pia kinapeleka umeme huko.
Uwekezaji wa Hongkong ni sehemu kubwa kabisa ya uwekezaji kutoka nje mjini Shenzhen, ambao unachukua asilimia 70 ya uwekezaji wote kutoka nje. Na mashirika ya Hongkong yanachukua asilimia 80 ya mashirika yenye mitaji kutoka nje mjini humo.
Sekta ya utamaduni ya mji wa Shenzhen inastawi siku hadi siku. Mjini humo kuna mashirikisho kumi ya waandishi na wasanii ambayo yana wajumbe 3464.
Katika mashindano ya miji inayoonekana kama bustani yanayongozwa na shirikisho la usimamizi wa bustani na burudani duniani(IFPRA), mji wa Shenzhen ulipata nafasi ya kwanza katika miji yenye watu zaidi ya milioni 1. Na uliteuliwa kuwa mmoja wa miji 500 yenye mazingira mazuri duniani na shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).
Hivi sasa eneo la kilomita za mraba 999.85 mjini humo linafunikwa na miti na majani. Na eneo la hifadhi ya kimaumbile ni kilomita za mraba 170.3, ambalo linafunika asilimia 8.7 ya eneo lote la mji huo.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-12
|