Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-13 16:24:50    
Mishumaa ya Shughuli Mbalimbali

cri

Ni kawaida nchini China kutumia mishumaa iliyopambwa nyakati za shughuli kama vile harusi, sherehe za kuzaliwa na mazishi. Mishumaa iliyotengenezwa kusini mwa mkoa wa Jiangsu ni maarufu sana kutokana na mabombwe yake ya kupendeza na ustadi wa kuitengeneza na mpaka sasa bado inatumiwa sana na wakulima wa huko.

  

Mishumaa myekundu hutumiwa nyakati za sherehe za furana na myeupe kwa ajili ya mazishi. Sehemu ya juu ya mshumaa hupambwa kwa maua yaliyotengenezwa kwa nta au karatasi ngumu yenye utando wa nta na kioo kidogo chenye maneno mbalimbali kwa mujibu wa tukio lenyewe, kama vile "Baraka za joka na phoenix", "Ndoa yenye maelewano itakayodumu kwa karne moja" au "Uishi milele kama Milima ya Kusini". Sehemu ya kati ya mshumaa ambayo ndiyo mwili wa mshumaa wenyewe hutiwa mabombwe ya majoka yanayochzea mipira ya dhahabu au phoenix wanaorukaruka kwenye maua ya peony na kuongezewa madoido ya vyura wenye miguu mitatu na vipepo.

  

Mishumaa inayotumiwa kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa hupambwa Mungu wa Maisha Marefu au kulungu na korongo ambao wote ni ishara ya maisha marefu. Mishumaa myeupe kwa ajili ya misiba hunakshiwa kwa maua ya mfuto na huandikwa maneno machache ya kumuomboleza marehemu. Aghalabu mapambo ya sehemu ya chini ya mshumaa huwa yanasimulia hadithi za paukwa pakawa kama vile "Makaika Wanane Wavuka Bahari" na "Liu Hai Amvua Mizuka wa Chura".

  

Utengenezaji wa mishumaa iliyopambwa unachanganya sanaa ya kukata karatasi, uyeyushaji nta, uchanganyaji rangi, kusubu na uchoraji. Jozi ya mishumaa iliyonakshiwa kutengenezwa na mtengenezaji mishumaa mahiri.

Zana za kutengeneza mishumaa ni pamoja na za kuyeyusnia nta, michapo ya metali, brashi za kuchorea na kalibu za mbao, shaba na towe. Mali ghafi inayotumiwa ni nta au shahamu, rangi, karatasi za rangi, shanga za kioo na waya.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-13