Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-20 14:39:24    
Historia ya Ukimwi (1)

cri

Maandishi kuhusu Ukimwi yalianza mwaka 1981, na kabla ya hapo binadamu walikuwa hawaufahamu hata kidogo ugonjwa huo. Hatuna uhakika kuwa katika miaka ya 70 ya karne iliyopita au zamani zaidi watu wangapi walikufa kutokana na ugonjwa huo, walikuwa hawajui chanzo cha utonjwa huo wala hawakuufahamu ugonjwa wenyewe, mazungumzo yalikuwa mengi lakini yote yalikuwa hayana msingi wa kisayansi, na hakuna gumzo hata moja lililokubalika kwa wote.

Virusi vya Ukimwi viliwashambulia binadamu kimya katika hali ambapo binadamu walikuwa hawajajiandaa, kisha vikaenea bila binadamu kujihadhari navyo. Mtaalamu mmoja wa Ukimwi alieleza, maambukizi ya ugonjwa huo katika kipindi cha mwanzo kwa neno "kimya". Baadaye tuligundua kwamba virusi vya ugonjwa huo vinaharibu viungo vya mtu na kumfanya apoteze uwezo wa kujikinga na magonjwa.

Mwezi Machi na Aprili, mwaka 1981 magonjwa mawili yaliwatahatharisha wataalamu wa kituo cha udhibiti maabukizi ya ugonjwa nchini Marekani, moja ni nimonia ya scysticercu na mwingine ni uvimbe fulani mwilini, magonjwa hayo yalitokea miongoni mwa mashoga wa kiume mjini New York. Wakati huo wagonjwa nimonia ya scysticercu pia waligunduliwa katika mji huo na jimbo la Califonia. Wagonjwa hao walipona au walikufa baada ya siku kumi.

Tarehe 5 Juni, kituo cha udhibiti maabukizi ya ugonjwa cha Marekani kilitoa habari kuhusu "nimonia ya cysticercus" kwenye jarida la "Ripoti ya kila wiki kuhusu kiasi cha watu waliopata na waliokufa kwa ugonjwa huo", kisha madaktari wa sehemu mbalimbali walipiga siku wakisema kuwa wamegundua ugonjwa huo katika sehemu zao.

Watu wanaona kuwa makala hiyo ni dalili ya kutokea kwa Ukimwi, na ni mwanzo kabisa wa binadamu kuufahamu Ukimwi.

Mwanzoni, watu walikuwa hawajui chanzo cha magonjwa hayo, waliona pengine yalisababishwa na dawa za kulevya, lakini magonjwa hayo yanaambukiza miongoni mwa mashoga wa kiume tu na hayaathiri watu wengine, kwa hiyo yalipuuzwa. Lakini baada ya miezi mitano kupita wazo lao hilo likathibitishwa kuwa ni kosa. Mgonjwa wa kwanza aliyetumia dawa za kulevya kwa sindano aligunduliwa, hii inaonesha kwamba ugonjwa huo licha ya kuambukiza miongoni mwa mashoga wa kiumme bali pia watu wengine, wakati huo kulikuwa na habari kuwa mwezi Desemba mwaka 1981 Ukimwi ulikukwa umevuka Atlantiki na kuingia nchini Uingereza. Tokea hapo wingu hilo jeusi lilianza kuzunguka zunguka barani Ulaya.

Mwezi Julai, mwaka 1982, wagonjwa wa Ukimwi waligunduliwa katika majimbo 23 nchini Marekani na waliongezeka na kufikia 452. Kutokana na ongezeko la wagonjwa watu walianza kufahamu njia yake ya maambukizi.

Mwaka 1982 mtoto mmoja ambaye hakutimiza umri wa miaka miwili aliambukizwa Ukimwi kutokana na kuongezwa damu mara nyingi. Hii inamaanisha kuwa ugonjwa huo unaambukiza kwa damu, katika mwaka huo huo kituo cha udhibiti wa maambukizi ugonjwa cha Marekani kiligundua mtoto mchanga aliambukizwa na Ukimwi na mama yake.

Katika siku ambapo watu walijaribu kuelewa ugonjwa wenyewe walikuwa wakitafuta jina la ugonjwa huo.

Mwezi Agosti, 1982 jina la ugonjwa huo lilibainika kwa ufupi AIDS, kwa ufupisho wa Kiswahili ni UKIMWI yaani upungufu wa kinga mwilini. Na jina hilo linaendelea kutumika hadi sasa. Jina hilo linamaanisha kuwa ugonjwa huo ni mkusanyiko wa magonjwa ambao wagonjwa tofauti wanaonekana kwa hali tofauti. Lakini msingi wa ugonjwa huo ni kupoteza uwezo wa kujikinga na magonjwa mwilini.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-20