Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-20 15:49:15    
Mchoraji maarufu Huang Zhou

cri

Huang Zhou ni mchoraji hodari wa picha za watu na wanyama. Michoro yake inayowapa watazamaji kumbukumbu nzuri ni ile inayoonyesha mila na desturi za wenyeji wa Xinjiang.

Miaka ya 1950, Huang Zhou akiwa mchoraji wa jeshini aliishi huko Xinjiang kwa miaka kadhaa. Maisha ya makabila mengi madogo madogo ya huko yalikuwa ni ujumbe muhimu wa kudumu katika michoro yake. Mila na desturi za Xinjiang huwa ni taswira ya michoro yake, wanaume na wanawake, wazee na watoto, walio wachangamfu na wenye furaha, na wanyama wa kupendeza kama vile punda, ngamia, farasi na kondoo, ndio wahusika wakuu wa michoro yake.

Huang Zhou ana tabia ya uchangamfu, uwazi na anapenda mawasiliano ya kirafiki, maisha ya amani, ngoma, nyimbo na furaha. Michoro yake ni adilifu, yenye hisia za dhati na kishairi.

Alipokuwa kijana, Huang Zhou alianza kufuatiliwa katika fani ya uchoraji kutokana na mtindo wake mpya. Hakupata fursa ya kusoma katika chuo cha sanaa, lakini baadaye amekuwa mchoraji mwenye taathira kubwa katika fani ya uchoraji ya zama hii ya China, kutokana na kipaji, bidii na moyo wake wa uvumbuzi bila kufuata kikasuku kanuni za zamani.

Yeye anaelewa fika jadi ya sanaa ya uchoraji wa michoro ya Kichina na pia alijifunza kwa dhati mbinu za uchoraji wa Kimagharibi, lakini jambo muhimu ni kwamba katika mazoezi ya miaka mingi ya uchoraji umejjengea mtindo mpya wa kutumia brashi na wino. Mtindo huo wa pekee umechanganya vyema mbinu za kutumia brashi na wino na tabia bora za mchoraji Mtindo huo ni mchango wa Huang Zhou katika kuendeleza, uchoraji wa Kichina.

Katika mawazo ya watu, Huang Zhou anajulikana kwa michoro yake ya punda. Huang alizaliwa mwaka 1925 katika wilaya ya Lixian, mkoani Hebei. Huko kuna punda wengi na Xinjiang vilevile ni mahali kwenye punda wengi. Kuchora punda lilikuwa wazo lake la mwanzo la kujifunza mbinu ya kutumia brashi na wino. Uchoraji huo ulimletea mafaniko makubwa na sasa michoro yake ya punda imekuwa sanaa bora ya pekee.

Huang Zhou pia ni mtunzaji na mthibitishaji wa michoro na vitu vya kale. Kati ya vitu alivyovitunza zipo maandiko ya kisanaa na michoro iliyochorwa na wachoraji mashuhuri wa Enzi ya Tang, Song, Ming, Qing na zama za karibuni, samani za Enzi ya Ming, michongo ya jade ya vipindi vya Shang Zhou, Madola yaliyopigana na Chunqiu na ya enzi za Han, Song, Ming na Qing na mihuri ya mawe na vyombo vya kauri vya enzi za Song, Yuan, Ming na Qing, karibu kila moja ni hazina ya dunia.

Huang alijenga jumba la sanaa la Yuanhuang kwa ajili ya kuvitunza vitu vyake na kuvionyesha mara kwa mara kwa wananchi. Jumba hili pia limekuwa mahali pa kuonyesha sanaa bora za zama hizi na kubadilishana maarifa ya sanaa kwa wasanii.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-20