Katika mkahawa wa chakula cha kithailand mjini Beijing Phrik Thai, mwandishi wetu wa habari aliona kuwa wahudumu wa Thailand waliovaa nguo za jadi za Thailand wakimsalimia kila mteja kwa kithailand, ambapo hali nzito ya kithailand ilionekana dhahiri kwenye mkahawa huo. Kwenye mlango wa kuingia kwenye ukumbi wa kulia chakula, kuna ukuta mmoja usio na mapambo yoyote, juu yake kuna sanamu moja ya mawe ya kichwa cha Buddha iliyoletwa China kutoka Thailand ilitiwa ndani ya ukuta. Kwa kumulikiwa na taa, maji yanayotiririka yanapita kwa utaratibu kwenye uso wa sanamu, halafu maji hayo yanaingia kiajabu ndani ya mkahawa huo.
Mteja mmoja Dada Su Xue alimwambia mwandishi wa habari wakati wanapokula chakula, waliweza kusikia sauti ya mtiririko wa maji, huku wakijihisi kama wamefika nchini Thailand na kula chakula kando ya mto. Mwendeshaji wa mkahawa huo Bwana Lu Weiming na mtu wa Hong Kong, China, yeye ni mtaalamu wa kusanifu na kupamba nyumba. Alimwambia mwandishi wa habari akisema:
Anapenda kutumia mtiririko wa maji kuonesha mandhari ya maumbile ya mto wa Thailand na kuonesha utamaduni wa mito wa Thailand. Thailand ni nchi inayotilia maanani zaidi maendeleo ya kilimo, na chanzo cha utamaduni wa nchi yenye maendeleo huanzia mito.
Ili kuonesha hali asilia kabisa ya Thailand, zana na vifaa vingi vya ujenzi wa mkahawa huo wa kithailand vililetwa kwa ndege nchini China kutoka Thailand.
Katika mkahawa huo, taa zote ni za mbao, mwanga wake ni laini na giza kidogo, ambapo meza moja moja zenye mtindo wa kupendeza zinaonesha hali ya utulivu na masikilizano. Katikati kuna kibanda kimoja kinachoweza kutumiwa na wateja zaidi ya 10 kwa pamoja, ambacho kilijengwa na Bwana Lu kwa kufuata mtindo wa vibanda vilivyoko kando ya barabara nchini Thailand. Bwana Lu alisema:
Nataka kujenga mazingira ya kimaumbile katika mkahawa ili wateja wakila hapa, waweze kujisikia hali ya mazingira ya kimaumbile nchini Thailand.
Katika mkahawa huo, kuna vyumba vidogo vitano vya kulia, kila chumba kinapambwa kwa mtindo wake maalum. Kimoja kati yao kilipambwa kwa kufuata hali ya nyumbani kwa wathailand. Mke wa Bwana Lu bibi Norah alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, kila akiingia kwenye chumba hicho cha kulia huona kama amerudi nyumbani kwake nchini Thailand.
Nikiingia kwenye chumba hicho huona kama nimerudi nyumbani kwangu Thailand, ndani yake kuna kitanda, na meza moja ya chakula. Napenda sana kulia chakula kwenye chumba hicho.
Mkahawa huo unawahudumia wateja chakula mbalimbali cha mtindo halisi wa kithailand, hata vitu vingi vya kupikia chakula vilichukuliwa kutoka Thailand, na wapishi wote pia ni wathailand, hivyo vyakula walivyopika kweli ni vyakula halisi vya kithailand.
Katika mkahawa huo wa kithaland, wateja wanakula chakula, huku wakiweza kupata fursa ya kutumbukizwa kwa nyimbo na dansi ya Thailand, na waimbaji na wachezaji dansi wote wanatoka Thailand.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-23
|