Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-26 16:21:31    
Maonesho ya kimataifa-Maonesho ya mavumbuzi ya kisasa

cri

Tokea mwaka 1851 maonesho ya kwanza ya kimataifa yafanyike mjini London hadi mwaka 2005 maonesho ya kimataifa ya Aichi yanayofanyika nchini Japan, miaka 154 imepita. Katika muda wa karne moja na nusu dunia imebadilika sana. Maendeleo ya binadamu na mabadiliko makubwa ya maisha bora hayawezi kutengana na uvumbuzi, na maonesho ya kimataifa yameandaa jukwaa la maonesho hayo ya uvumbuzi, na maonesho yenyewe ya kimataifa pia ni aina moja ya uvumbuzi.

Maishani mwetu, vitu ambavyo tumekwisha zoea kama taa, simu, gari, majumba marefu, vyombo vya angani na vitu vingine, vyote viliwahi kuoneshwa katika maonesho ya kimataifa kama ni uvumbuzi na kuwafahamisha binadamu na mwishowe vilitumika sana duniani. Tukifungua mafaili ya maonesho ya kimataifa, vitu toka raba, saruji, vyombo vya alumini, hadi charahani, toka saa ya kengele, taa ya umeme, simu ya upepo hadi mashine ya kuzalisha umeme na toka mashine ya mvuke, gari, ndege hadi chombo cha angani, wote huo ni uvumbuzi ulioharakisha maendeleo ya binadamu na kuweka msingi wa utamaduni wa kisasa, na yote hayo yaliwahi kuoneshwa katika maonesho ya kimataita.

Katika maonyesho ya kimataifa yaliyofanyika mwaka 1851 ulioneshwa uvumbuzi wa saa za kengele, mashine ya mvuke na sampuli za mahandaki na daraja, na kitu kilichovutia zaidi ni jengo lililotumia chuma cha pua tani 4500 na vipande vya vioo laki 3. Matumizi ya chuma cha pua pamoja na vioo yalifungua ukurasa mpya wa usanifu wa majengo yanayotumika hadi sasa.

Mwaka 1878, katika maonesho ya kimataifa mjini Paris ilioneshwa simu ya Bell na santuri ya Edison.

Hakuna mtu asiyejua Mnara wa Eiffel mjini Paris, mnara huo ulikuwa ni jengo muhimu katika maonesho ya kimataifa yaliyofanyika mjini Paris mwaka 1889.

Profesa mmoja wa Marekani aliwahi kusema "ukiwa mvumbuzi au mtengenezaji na unataka kuwafahamisha vitu vyako kwa watu, ni bora ushiriki na vitu vyako kwenye maonesho ya kimataifa."

Maonesho ya kimataifa ni jukwaa la kuonesha uvumbuzi, ni jukwaa la mafanikio mapya ya binadamu, na yanaonesha upeo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya nchi fulani na kusukuma mbele ustaarabu wa binadamu.

Tukiangalia mafaili ya maonesho ya kimataifa, kila maonesho yalikuwa na mada yake, lakini ukiangalia kwa ujumla yote yalionesha mabadiliko ya msimamo wa binadamu kwa mazingira ya maumbile. Tokea karne ya 20 tatizo la mazingira lilianza kuvutiliwa zaidi, maonesho yote yametilia mkazo: Binadamu watatunzaje mazingira na kukaa nayo kwa upatanifu.

Maonesho ya Aichi nchini Japani mwaka huu yalikuwa na mada hiyo ikisisitiza kuhifadhi mazingira na kujenga jamii yenye mandeleo ya uchumi unaotumia maliasili kwa mzunguko. Alama njema ya maonesho hayo ni miti miwili ya "babu wa miti" na "mwana wa miti".

Binadamu wamepata maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, wamepata jamii yenye starehe, lakini wanakabiliwa na mabadiliko mabaya ya hali ya hewa, upungufu wa maliasili, na mabadiliko ya ardhi kuwa jangwa. Ili kuhifadhi mazingira yetu na kupata ukuaji wa uchumi, na kuwaachia dunia nzuri wajukuu wetu, nchi zaidi ya 120 zilionesha mawazo yao ya aina mbalimbali kuhusu tatizo hilo.

Kama maonesho ya kimataifa yaliyopita, maonesho katika karne mpya yanatarajiwa yatoe mwongozo kwa binadamu namna ya kustawisha mazingira pamoja na maendeeo ya uchumi na kuwafanya binadamu wapatane na mazingira.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-26