Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa China Bw. Zhou qiang tarehe 23 alipohudhuria sherehe ya ufunguzi wa mashindano ya ufundi wa vijana wa China ya kombe la "Zhenxing" alisema kuwa, kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote kunahitaji watu wenye uwezo mbalimbali, hasa vijana wenye elimu ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu wanapaswa kutoa mchango wao.
Bw. Zhouqiang alisema kuwa,kutokana na maendeleo makubwa ya uchumi na jamii ya China, watu wenye ufundi maalumu wanahitajika sana nchini China. Kuendelea kwa viwanda vya aina mpya italeta mabadiliko makubwa ya viwanda vya zamani na maendeleo makubwa kwa aina mpya ya viwanda, hivyo mahitaji ya watu wenye uwezo mbalimbali na ufundi wa hali ya juu yanaongezeka sana. Wakati huo huo, ili China ikidhi mahitaji ya umoja wa uchumi wa dunia na kushiriki kwenye ushindani na ushirikiano wa kimataifa, watu wenye uwezo mbalimbali na ufundi wa hali ya juu ni hakikisho katika kutimiza lengo hilo.
Alisema kuwa, hivi sasa, watu wenye uwezo maalumu wa sayansi na teknolojia wana fursa, watu hawa wanasifiwa sana , kila mtu mwenye ufundi maalumu anatoa mchango kwa jamii, mbali na hayo mshahara wa wafanyakazi wenye ufundi maalumu unaongezeka siku hadi siku.
Bw. Zhouqiang alisisitiza kuwa, Umoja wa vijana wa China siku zote kinazingatia kazi za kuandaa vijana wenye ufundi wa aina mbalimbali. Miaka mingi iliyopita, ulifanya shughuli nyingi kwa nyakati mbalimbali ili kutoa nafasi nzuri kwa vijana kuonesha uwezo wao katika maeneo mabli mbali. Ili kuanzisha njia mpya ya kuandaa wafanyakazi vijana wenye ufundi wa aina mbalimbali, kutokana na msingi wa uzoefu wa kazi za zamani, kamati kuu ya Umoja wa vijana wa China ilishirikiana na wizara husika kuanzisha mpango wa ukuaji wa uwezo na ufundi wa sayansi na teknolojia wa vijana katika mwaka uliopita.
Bw. Zhouqiang ana matumaini kuwa, jumuia mbalimbali za Umoja wa vijana wa China zinafanya kazi kutokana na mataka ya " mpango wa kimkakati wa kujenga taifa kwa kutumia watu wenye ufundi wa aina mbalimbali", kuandaa wafanyakazi vijana wenye ufundi wa hali ya juu.
Habari zinasema kuwa, katika mashindano ya ufundi wa vijana ya kombe la "Zhenxing" limewavutia vijana milioni 7.53 wamevutiwa kujiunga na shughuli hiyo.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-25
|