Mtaa wa utamaduni wa kale wa Liulichang mjini Beijing una historia ya miaka zaidi ya 100. Makumi ya maduka yanayouza vitu vya kale na sanaa za kila aina yanayopambwa kwa mapambo ya mitindo mbalimbali ya kale yamesambaa katika mtaa huo wenye urefu wa mita 1,000. Ukiingia kwenye duka lolote na kununua kitu chochote kinachoonekana kama cha kawaida, basi kitu hicho huenda kina historia ya karne kadhaa.
Mtaa huo ulijengwa upya mwanzoni mwa miaka ya 1980 ili kuwapa wageni mahali pa kuelewa utamaduni wa asili wa China. Maduka kwenye mtaa huo yana vitu vya sanaa vya aina nne: vitu vya sanaa vya kale, michoro na maandikio ya kisanaa, vifaa vya kuandikia, na vitabu vya kale. Wachina wanazidi kuongezeka miongoni mwa wateja wa maduka hayo, wananunua vitu hivi vya sanaa kwa sababu mbili: utunzaji wa mtu binafsi kutokana na ushabiki, na uwekaji akiba wa vitu hivyo ili kuepukana na kushuka kwa thamani ya pesa.
Ukiwa aina moja ya utamaduni, utunzaji wa vitu vya aina mbalimbali unazidi kuvuma mjini Beijing. Kutokana na takwimu zisizokamilika, watu zaidi ya milioni moja wa Beijing wanapenda kutunza vitu vya kale. Kutoka michoro na hati za sanaa, vyombo vya kauri na jade, michongo ya mianzi, miti na pembe za ndovu, vifaa vya kuandikia, mpaka vitabu vya kale na vitu vingine vya aina mbalimbali, ujuzi wa watunzaji kuhusu vitu hivyo unazidi kupanuka, hivyo kiwango cha kutunza na kukagua vitu vya utamaduni na vitu vya sanaa pia kinazidi kuinuka. Kufuatana na maendeleo hayo, kwa misingi ya masoko ya vitu vya utamaduni ya Liulichang na Hongqiao, Duka la Urafiki na maduka madogo yaliyoko ndani ya hoteli kubwa, kumetokea mahali pa minada ya vitu vya sanaa, ujia wa michoro na maonesho ya sanaa, ambapo pameunganisha vizuri sanaa na utunzaji.
Kati ya taasisi zinazoshughulikia harakati hizi, kampuni za kuendesha minada ya vitu vya sanaa ndizo zenye shughuli nyingi. Sasa, Beijing ina kampuni nyingi za minada, kama vile Hanhai, Jiade, Pasifiki na Shengjia, ambazo ingawa wateja wake hawafanani, lakini zote zina soko kubwa kutokana na sifa zao za kuhakikisha ukweli na kushikilia haki. Si katika minada mikubwa miwili ya majira ya mchipuko na mpukutiko kila mwaka, wala minada midogo ya kila mwaka, wala minada midogo ya kila mwezi inayohudumia watu wanaolipwa mishahara, asilimia ya biashara iliyofanyika ilikuwa kubwa na biashara yenyewe ya minada inazidi kupevuka.
Kupevuka kwa soko la vitu vya sanaa pia kuna maana muhimu katika kutunza vitu vya utamaduni vya taifa. Kutokana na minada, vitu vya sanaa vyenye thamani vilivyotunzwa na watu binafsi vilijulikana na kupata kutunzwa vizuri zaidi na vitu vya utamaduni vilivyopotelea ng'ambo vilirudi nchini.
Katika Mnada Maalumu wa vitu vya An Siyuan (mtunzaji maarufu na mfanyabiashara wa vitu vya kale wa Marekani) ulioendeshwa na kampuni ya minada ya kimataifa ya Shengjia mwaka 1995, vitu 81 vilivyonadiwa vilirudi China. Sasa, serikali ya China imekwishaweka sera kuhusu minada ya vitu vya utamaduni vya thamani.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-27
|