Ili kuendeleza elimu ya lazima kwa uwiano nchini China Wizara ya Elimu ya China hivi karibuni imetoa waraka wa "Maoni kuhusu Kusukuma Elimu ya Lazima kwa Uwiano". Waraka huo unazitaka idara za elimu za ngazi zote zikusanye juhudi kwenye kuendesha vizuri kila shule na kufuatilia vema ukuaji wa kila mtoto, na kwa mafanikio kudhibiti hali ya tofauti ya maendeleo ya elimu inayozidi kuwa kubwa kati ya shule na kati ya sehemu.
Ofisa wa Wizara ya Elimu alisema, msingi wa elimu ya lazima ni hafifu, na hali ya tofauti ya maendeleo ya elimu inazidi kuwa mbaya ikiwa pamoja na tofauti ya maendeleo ya uchumi, tofauti iliyopo ya elimu ya lazima ipo kati ya sehemu, miji na vijiji na kati ya shule. Na tofauti hizo zinajitokeza zaidi katika mazingira ya shule, fedha za shule na kiwango cha walimu.
"Maoni" yanaeleza kuwa ili kusukuma elimu ya lazima, kwanza ni lazima iwekwe kigezo cha kimsingi kinacholingana na hali halisi ya mazingira ya shule na kuchukua hatua za kupunguza tofauti hatua kwa hatua na kuhakikisha shule zenye hali duni zinapungua mwaka hadi mwaka. Shule za kiserikali ziwapokee watoto kujiunga na shule zilizo karibu nao bila mtihani, na ni marufuku kuzifanya shule fulani kuwa muhimu, hatua zichukuliwe ili kudhibiti uchaguzi wa shule katika kipindi cha elimu ya lazima.
Pili, serikali za wilaya zifanye mpango wa matumizi ya nyenzo za walimu wa wilaya yake, na kuimarisha misaada kati ya shule kupitia walimu wenye uzoefu kufundisha madarasa katika shule tofauti kila baada ya muda fulani, na walimu wanaoadimika wa elimu fulani wafundishe madarasa yao bila shule maalum, na walimu wa mijini wafundishe katika shule za vijijini kwa muda na kutoa msaada wa ufundishaji baina shule za mijini na shule za vijijini na kuwasaidia walimu wa vijijini wainue kiwango chao cha ufundishaji.
Tatu, utaratibu uwekwe ili kuinua ubora wa elimu ya kila shule. Hatua kwa hatua uanzishwe utaratibu wa kupima matokeo ya masomo ili kuhakikisha shule inandeshwa kwa kigezo kimoja katika elimu ya msingi. Kadhalika, hatua zichukuliwe ili wanafunzi maskini wasaidiwe zaidi na wapate maendeleo ya masomo sawa na wanafunzi wengine.
Nne, sera zote husika zitekelezwe ili kuhakikisha wanafunzi wenye hali mbaya kiuchumi wanapata elimu ya lazima. Na lazima zitekelezwe sera za kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia zinazosaidiwa na serikali wanasamehewa ada ya shule. Wanafunzi wa vibarua wa mijini kutoka vijijini watendewe sawa na wanafunzi wa mijini na matatizo ya wanafunzi waliobaki vijijini kutokana na wazazi wao kwenda mijini kufanya kazi za kibarua yatatuliwe na kuwasaidia kimasomo na kimaisha, na kuimarisha masomo kwa watoto walemavu.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-31
|