Hivi sasa nchini China wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu, wengi wao hujitahidi kutafuta idara zinazoweza kuwapatia nafasi ya kufanya mazoezi ya kikazi kabla ya kuhitimu masomo yao. Katika siku za hivi karibuni, Kamati kuu ya Umoja wa vijana na Wizara ya elimu ya China zilitoa "maoni kuhusu kufanya vizuri zaidi kazi kuhusu wanafunzi wanaofanya ajira ndogondogo kwa kujipatia ada na wanaofanya mazoezi ya kikazi kabla ya kuhitimu masomo", ambayo imewekwa kuwa malipo ya kazi wanazofanya wanafunzi wa vyuo vikuu yanapaswa kufikia yuan 8 za renminbi kwa saa moja. Mwandishi wa habari aliona kuwa, ni rahisi kwa makampuni mengi ya Beijing kutoa malipo hayo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya mazoezi ya kikazi, lakini makampuni madogo au ya wastani yanatoa malipo chini kidogo, kwani makampuni hayo yanaona kuwa wanafunzi wanakwenda makampuni hayo kutafuta nafasi ya kufanya mazoezi ya kikazi kwa hiari yao, hayawezi kuwapatia malipo ya juu. Na wanaofanya ajira ndogondogo katika mikahawa huweza kupata malipo ya juu kidogo. Mwandishi wetu wa habari alipowahoji wanafunzi, wengi wanaona kuwa, wanayozingatia zaidi ni kuhusu nafasi ya kufanya mazoezi ya kikazi, na bora wapate nafasi ya kufanya mazoezi ya kikazi katika makampuni makubwa, hata hawajali sana malipo wanayoweza kuyapata.
Xiao Zhao anayesoma kozi ya habari katika chuo kikuu kimoja cha Beijing amefanya mazoezi ya kikazi kwa miezi mitatu katika shirika moja la gazeti, alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa, mwanzoni hata hakufikiri kuhusu malipo ya kazi, ila tu kujitahidi kujipatia nafasi ya kufanya mazoezi ya kikazi. Na shirika hilo la gazeti lilitoa malipo kutokana na kazi alizofanya. Xiao Zhao anaona kuwa, amepata nafasi hiyo ya kufanya mazoezi ya kikazi kabla ya kuhitimu masomo ni kwa ajili ya kuongeza ujuzi, wakati wa kufanya mazoezi ya kikazi, alisaidiwa na wafanyakazi wa shirika la gazeti hilo, alipata uzoefu mwingi na kutambua upungufu wake mwenyewe, na amekazi nia ya kujifunza kwa juhudi kubwa zaidi ili siku za usoni atafanya vizuri kazi atakayopata. Alisema kuwa, malipo ya kazi si muhimu kwake, na uzoefu na maarifa anayopata katika mazoezi ya kikazi ni muhimu zaidi.
Ofisa wa Kampuni ya SIMENS anayeshughulikia mambo ya kuandikisha wafanyakazi katika vyuo vikuu Bi.Sun alijulisha kuwa, wanafunzi wa vyuo vikuu mjini Beijing waliofanya mazoezi kwenye kampuni ya SIMENS wanaweza kupata malipo ya yuani 80 kwa siku, mbali na hayo , kampuni hiyo inaweza kuwapatia huduma mbalimbali kama wafanyakazi wake rasmi walivyopata.
Kutokana na mazoezi ya kikazi na ajira ndogondogo walizofanya, wanafunzi wa vyuo vikuu kweli wamepata uzoefu na maarifa.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-03
|