Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-03 20:20:42    
Afrika yatumai kuimarisha ushirikiano ya madini kati yake na China

cri
    Afrika ni bara lenye maliasili nyingi, uwingi wake wa madini unachukua nafasi ya kwanza katika mabara yote duniani. Mwezi Februari mwaka 2004, mawaziri wa madini wa nchi 28 za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Ghana, Msumbiji, Sudan, Misri, Namibia, Botswana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong, walikutana huko Cape Town, kwenye mkutano wa 9 wa uendelezaji wa kazi za madini barani Afrika. Katika mkutano huo, mawaziri hao walieleza kuwa, Afrika inayakaribisha mashirika ya kigeni kuwekeza vitega uchumi katika kazi za madini kwenye bara hilo. Mawaziri hao walisema kuwa, Afrika ina madini mengi, na maliasili hizo zinapaswa kuwa sehemu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi katika bara hilo.

    China na Afirka zimedumisha urafiki wa jadi kwa muda mrefu. Serikali ya China imekuwa ikitilia maanani sana uhusiano wa kirafiki kati yake na nchi za Afrika, katika miaka mingi iliyopita, China imeipatia nchi nyingi za Afrika misaada mikubwa ya kiuchumi bila ya masharti yoyote. Hali ambayo imeweka mazingira mazuri kwa mashirika ya China kuingia kwenye masoko ya Afrika. Mbali na hayo, katika miaka ya hivi karibuni, ili kuhimiza na kusaidia mashirika ya China kuanzisha shughuli katika Bara la Afrika, idara zinazohusika za serikali ya China zimeanzisha vituo vya kuhimiza uwekezaji wa vitega uchumi katika nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Misri, Cameroon, Mali, Guinea, Cote d'Ivoire, Gabon, Tanzania, Zambia, Msumbiji na Nigeria. Vituo hivyo vimesaidia sana mashirika ya China yaliyoanzisha shughuli zao katika nchi za Afrika.

    Hivi sasa China imewekea vitega uchumi nchini Tanzania, Sudan, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Afrika ya Kusini katika nyanja za uendelezaji wa maliasili za madini.

    Afrika ya Kusini si kama tu ni nchi yenye madini mengi ya dhahabu duniani, bali pia inamadini mengi ya chuma. Hivi sasa viwanda viwili vya chuma na chuma cha pua vya China vimewekeza nchini Afrika ya Kusini. Kampuni ya kundi la viwanda na biashara la chuma na chuma cha pua ya China ilianzisha kampuni ya maliasili ya madini ya Asia ya Afrika ya Kusini mwezi Desemba, mwaka 1995 ambayo inaendesha shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma na uyeyushaji wa madini ya chuma. Kampuni hiyo ni ya ubia, upande wa China unadhibiti hisa. Na kampuni ya chuma na chuma cha pua cha Jiuquan cha China pia inafanya mpango wa kuanzisha shughuli zake za kuchimba madini ya chuma nachromium. Nchini Afrika ya Kusini.

    Mbali na uwekezaji vitega uchumi, biashara ya madini kati ya China na nchi za Afrika inakua kwa haraka. Naibu mkurugenzi wa Jumuiya ya Biashara ya Nje ya Madini nchini China Bw. Wang Yuanjiang alieleza kuwa, thamani ya biashara ya madini kati ya China na Afrika kwa mwaka 2004 ilifikia dola za kimarekani bilioni 14, na kuongezeka kwa asilimia 74.8 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2003.

    Bw. Wang Yuanjiang alisema kuwa, biashara hiyo ya madini inanufaisha pande zote za China na Afrika. China inaziuzia nchi za Afrika bidhaa zinazohitaji kama vile vifaa vya chuma na chuma cha pua, matairi, na vitu vidogo vidogo vya kimadini, na China inanunua kutoka kwenye nchi hizo mafuta, mawe ya madini na vito zinazomilikiwa nyingi na nchi hizo. Bw. Wang Yuanjiang alieleza kuwa, Afrika ina madini mengi, na China inaendelea kwa haraka. Hivyo biashara hiyo kati ya pande hizo mbili ina mustakabali mzuri zaidi siku za usoni.

    Bw. Wang Yuanjiang alieleza kuwa, nchi nyingi za Afrika zinatarajia kusukuma mbele maendeleo ya uchumi, kupitia ushirikiano wa kichumi na kibiashara na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo madini. Kwa upande mwingine, China pia inahitaji ushirikiano huo muhimu na Afrika. Hivyo alisema kuwa ana imani kubwa kwamba, ushirikiano huo utaendelea vizuri katika siku za baadaye.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-03