Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-03 20:45:34    
Utarizi wa Dantu

cri

Mji wa Zhenjiang, mkoani Jiangsu ni mji maarufu kwa historia na utamaduni nchini China. Mji huo uko kwenye eneo la makutano ya Mto Changjiang na Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou. Sanaa za huko ni maridhawa.

Utarizi kwenye nguo na vitu vingine vya maisha unaoenezwa katika Kitongoji cha Nanxiang, wilayani Dantu una mtindo maalumu. Mabombwe mazuri ya watu, maua, nyasi. Wadudu, samaki, ndege, wanyama au maneno yanayomithilisha maana maalumu, hutarizwa katika vimori, vitambaa vya kuhifadhia mabega ya watoto, kola, mapindo ya mikono ya nguo za wanawake, foronya za mito za maarusi na nguo za mitindo ya wazee.

Utarizi wa huko una hulka ya kuwa na mshono kingama kwenye nguo. Kwa kawaida haufuati taswira bali unashonwa kwa kutazama vitu halisi tu. Mshono huo una njia, mitindo ya mistari na ombwe. Mabombwe ya mshono kingama na utarizi huria huwa yanabadilikabadilika, pia yana mipangilio sawa na mvuto wa kisanaa wa taswira. Kazi nyingi za mabombwe hayo maalumu huko Dantu zinafumwa kwa kutegemea mawazo ya kinamama werevu. Kwa mfano kitambaa kimoja cha kuhifadhia mabega ya mtoto chenye umbo la yungiyungi kinaweza kushonwa kwa kuunganisha petali 16. Kila petali inatarizwa maua tofauti, kwenye baadhi ya petali hutarizwa vichwa vya watoto vinavyojitokeza. Hii inamithilisha kuwa mtoto atakayevaa kitambaa hicho atapendeza kama maua.

Mabombwe ya utarizi ya Dantu hutarizwa maua, ndege, watu na wanyama katika mandhari moja. Rangi kuu zinazotumiwa ni nyekundu, kijani na manjano ambazo zinaonyesha mtindo wa kienyeji.

Utarizi wa Dantu hauoneshi umakini wa utarizi wa Suzhou na Hunan, lakini unawavutia watu kwa namna yake rahisi ya kiasili.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-03