Tarehe 25 mwezi Mei, naibu spika wa bunge la umma la China, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa China Bi. Gu Xiulian alifungua rasmi tovuti ya uhamiaji wa nguvukazi za wanawake wa China (www.womenldl.com.cn).
Hivi sasa kwenye tovuti hiyo, wanawake milioni 2.52 wametoa maombi ya kazi, kuna nafasi elfu 80 za ajira zilizotolewa na idara na viwanda mbalimbali zinazowafaa kina mama, na kuna habari nyingi zinazohusika kama vile mwongozo wa kazi, sera na utaratibu, maingiliano ya kazi, mahitaji ya kazi na utoaji ajira.
China ina raslimali nyingi ya nguvukazi, ni asilimia 37.6 tu ya idadi ya Wachina wanaishi mijini, vijijini kuna nguvukazi kubwa ya ziada, ambayo theluthi moja ni wanawake. Takwimu zilizotolewa na mashirika ya wanawake ya sehemu mbalimbali nchini China zinaonesha kuwa, hivi sasa wanawake wa China wanaotafuta ajira wamefikia milioni 2.52, na makampuni na viwanda vya sehemu za pwani vinahitaji vibarua zaidi ya elfu 80.
Ili kuwasaidia wanawake wa mijini na vijijini kubadili au kupata ajira, kuanzisha mawasiliano kati ya viwanda, mashirika ya wanawake na kina mama wanaotafuta kazi, kunavisaidia viwanda kutatua suala la upungufu wa nguvukazi, na kuwasaidia wanawake kupata ajira, Umoja wa Wanawake wa China uliamua kuanzisha tovuti ya nguvukazi za wanawake chini ya uungaji mkono wa wizara ya sayansi na teknolojia , wizara ya kazi na huduma za jamii, wizara ya kilimo , na shirikisho la wafanyakazi na wafanyabiashara la China.
Tovuti hiyo itakusanya habari kwa njia mbalimbali ili kuimarisha soko la ajira.
Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa China, ambaye pia ni makamu wa kwanza wa katibu mkuu wa ofisi ya Sekretarieti ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bi. Huang Qingyi kwenye ufunguzi huo alisema kuwa, tovuti hiyo itasaidia nguvukazi za ziada za wanawake wa vijijini kupata ajira kwa urahisi mijini , itakuwa daraja linalounganisha nguvukazi za ziada za wanawake, mashirika ya wanawake na idara zinazohitaji nguvukazi.
Bi. Huang Qingyi alisisitiza kuwa, ili kuifanya tovuti hiyo iwe na umaalum wake, na kuwahudumia vizuri kina mama, inapaswa kuweka mkazo kukusanya habari kwa makini, kuongeza na kubadilisha habari kwa wakati, kutajirisha mambo yaliyomo na kuifanya iwe njia mwafaka kwa kina mama kupata habari husika na ajira wanazotaka.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-03
|