Katika sehemu ya utalii ya Yangtaishan karibu na Beijing, kwenye matawi ya miti mifuko ya plastiki inapeperushwa na upepo, na kwenye ardhi yenye majani mabichi karatasi za kufungia chakula zinaonekana hapa na pale, na kati ya majabali kuna makopo na chupa za vinywaji. Hii ni mandhari inayosikitisha machoni mwa watu waliojitolea kuokota takataka katika sehemu hiyo ya utalii.
Tarehe 5 yaani "siku ya mazingira duniani", watu mia moja kutoka sekta mbalimbali walijitolea kuokota takataka hizo.
Takataka zilizotupwa na binadamu maishani mwao sio uchafuzi tu katika sehemu za utalii bali pia ni uchafuzi unaoenea kila mahali, limekuwa suala la jamii linalofuatiliwa sana. Tarehe 4 Mei, mwaka 2005 Shirika la Simu za Mkononi TCL na Shirikisho la Hifadhi ya Mazingira la China katika muda wa siku 40 yalikusanya maoni milioni 4 yaliyotumwa kwa simu za mkononi kuhusu "suala linalofuatiliwa zaidi kuhusu mazingira safi", matokeo yalionesha kuwa tatizo la takataka zilizotupwa maishani mwa binadamu ni kubwa likifuatia matatizo ya uchafuzi wa maji na hewa.
Mkuu wa Idara Kuu ya Hifadhi ya Mazingira ya China alisema kuwa katika miaka ya karibuni, sekta ya utalii imeimarika nchini China sehemu nyingi za utalii pamoja na maeneo yaliyo pembezoni mwa sehemu hizo, yamechafuka vibaya kutokana na takataka zilizoachwa na watalii. Katika tarehe 6, siku ya mazingira duniani, kazi ya kuwashirikisha watu mia moja kuokota takataka katika sehemu hiyo ya utalii kwa kujitolea ina lengo la kuwakumbusha watu wawe waangalifu wa kuhifadhi mazingira, na kuwataka watu wahifadhi mazingira "waanzie mambo madogo wanayopuuza, waanze kuacha mambo waliyokuwa nayo kila siku na waanze kutoka kwenye nafsi zao". Mmoja kati ya watu waliojitolea aliyetoka Shirika la Umeme alisema, akiwa kijana ana jukumu na wajibu kutoa mchango wake kwa ajili ya usafi wa mazingira, anatumai kazi hii itawahamasisha watu wengi watilie maanani hifadhi ya mazingira na waitunze vizuri dunia yetu. Mtu mwingine aliyetoka kutoka vyombo vya habari alisema, aliposikia kuna kazi hiyo ya watu waliojitolea kuokota takataka alitaka kujiunga nao, kwani anaona zoezi hilo lina maana sana.
Kazi hiyo ya kuokota takataka milimani iliandaliwa na Idara Kuu ya Hifadhi ya Mazingira na Shirikisho la Hifadhi la Mazingira la China, watu zaidi ya mia moja kutoka nyanja mbalimbali walishiriki kwenye kazi hiyo. Mada yake ilikuwa ni "tumia mikono yako kusafisha dunia yetu". Watu waliojitolea walipopanda na kushuka kutoka milima waliokota takataka zilizoachwa na watalii. Wao waliomba wapenda utalii na wapanda milima, "Usiondoke na chochote ila kumbukumbu nzuri, na usiache chochote ila alama za nyayo!" Na walitoa wito kwa wote kuwa tushikamane, tuache tabia mbaya, tupende maumbile na tuhifadhi mazingira?tuishi katika mazingira yenye milima, maji bila kuchafuka na hewa safi.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-08
|