Hivi sasa nchini Ujerumani kuna wagonjwa na watu wenye virusi vya Ukimwi karibu elfu 44, ni nchi yenye wagonjwa wachache wa Ukimwi duniani. Mtaalamu mmoja wa udhibiti wa Ukimwi wa Ujerumani alipojibu maswali ya waandishi wa habari alisema, mkakati wa kukinga na kudhibiti Ukimwi unasisitiza kueneza elimu kuhusu Ukimwi na kuinua mwamko wa waathirika wa kuchukua jukumu kwa nafsi yake na mwingine.
Bw. Robert, mtaalamu wa Ukimwi katika Kituo cha Kudhibiti Maambukizi ya Magonjwa nchini Ujerumani alisema kuwa hivi sasa sekta mbalimbali nchini Ujerumani zote zimeelewa kuwa ni lazima ziwaelimishe watu wawe na elimu kuhusu Ukimwi na kuwafanya waache vitendo vya hatari kwa hiari. Mwaka 2004 Ujerumani ilitenga Euro milioni 9 kwa ajili ya shughuli za kueneza elimu kuhusu Ukimwi.
Katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi, Ujerumani inatilia mkazo kuinua mwamko wa kila mtu kuchukua jukumu kwa nafsi yake na kwa wengine. Mtaalamu alisema, ni muhali kupata lengo la kudhibiti maambukizi ya Ukimwi kwa juhudi za serikali kudhibiti na kuwapima watu katika sehemu kubwa. Njia inayofaa ni kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi na wenye virusi wawe na mwamko wa kuchukua jukumu kwa nafsi zao, kuwafanya wafahamu hatari ya maambukizi na wajue namna ya kujikinga, na kuacha ngono zembe, ili wagonjwa na wenye virusi vya Ukimwi wengi wachukue jukumu kwa nafsi zao na kwa jamii. Sambamba na hayo ni kufanya uenezi wa elimu kuhusu Ukimwi kuwafahamisha wananchi namna ya kujikinga, na kuondoa dukuduku yao na kukaa vema na wagonjwa na wenye virusi vya Ukimwi.
Mtaalamu Robert alisema, kama ilivyo katika nchi nyingine wagonjwa na wanaoishi na virusi vya Ukimwi pia wanabaguliwa nchini Ujerumani, lakini nchini humo kuna nidhamu kali za kulinda hali za watu hao zisijulikane, ni vigumu kwa wengine kufahamu habari zao.
Ngono na matumizi ya dawa za kulevya ni njia muhimu ya kuambukiza Ukimwi. Katika jamii ambayo ni rahisi kuambukizwa Ukimwi juhudi kubwa za kueneza matumizi ya kondomu zilifanyika na serikali inatoa huduma bure ya kutumia sindano mara moja tu. Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa huduma hiyo inaweza kusababisha watu wengi kutumia dawa za kulevya kwa njia ya sindano. Kuhusu tatizo hilo Ujerumani ilifanya utafiti wa aina nyingi, matokeo yake ni kuwa huduma hiyo haiwezi kusababisha ongezeko la watumiaji dawa za kulevya na haiwezi kuwafanya watu ambao hawakutumia dawa za kulevya hapo awali waanze kutumia.
Imefahamika kuwa nchini Ujerumani kuna vituo vya udhibiti wa Ukimwi katika sehemu mbalimbali za mitaa, vituo hivyo vinagharamiwa kifedha na serikali na kazi zake ni kuwasaidia waathirika. Katika sehemu hizo za mitaa kuna vituo vya afya, vituo vya kuwasaidia wagonjwa wa Ukimwi, na vituo vya kutoa ushauri kuhusu Ukimwi, kama yakitokea matatizo ya kijamii na ya kiuchumi watu wanaweza kuomba misaada kutoka vituo hivyo. Kati ya vituo hivyo, kila kimoja kina kazi yake mahsusi na pia vinashirikiana, kwa kufanya hivyo medani ya kukinga na kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi imekuwa imara.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-10
|