Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-10 19:45:43    
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bwana Chirau Ali Mwakwere tarehe 8 afika Beijing kwa ziara ya siku 5 nchini China

cri

Mwandishi: Leo utakwenda Shanghai baada ya kumaliza ziara hapa Beijing?

Waziri: Nitakwenda Shanghai kuendeleza na ziara. Nimeambiwa kuwa huko kuna maendeleo ya juu sana ya viwanda na biashara, na kwa vile nchi zinazoendelea zinategemea sana biashara, ni jambo muhimu tujue nchi ya China ina vitu gani ambaavyo Afrika yaweza kununua, na ni vitu gani ambavyo wachina wanaweza kuvinunua kutoka Afrika hasa kutoka Kenya, kwa sababu sisi na wachina, uhusiano wetu umekuwa bora zaidi kwa sababu tuna biashara za kuendelea, mfano ni kuwa China imeruhusu Shirika la ndege la Kenya kuleta ndege zao mpaka Shanghai, hii ni hatua ambayo itakuwa na manufaa makubwa sana kwa watalii na wafanya bishara kutoka nchi zote mbili, na safari hizi za ndege ambazo kwa hivi sasa zafika mpaka Hongkong. Itakuwa imefungua nafasi kwa wafanya biashara na watu wengine wanaotaka kutembelea China au wachina wanaotaka kutembelea Kenya kwa utalii kwa ajili ya kusafiri rahisi zaidi. Ningependa kueleza kuwa, kati ya uhusiano wetu na China tunaweza kupata manufaa kwa vijana wavulana na wasichana kupata mafunzo kadha wa kadha, kama vile elimu, daktari, uhandisi na hata michezo katika nchi hii ya China. Hii inaletea karibu kabisa kama watu wakishirikiana kwa mambo yote ya maendeleo ya nchi na watu binafsi, hili ni jambo la kuridhisha sana.

  Mwandishi: Umepata picha gani juu ya Beijing?

Waziri: Beijing ni mji safi sana. Wananchi wa hapa hali yao ya nidhamu iko juu sana, sijaona takataka zozote hata kijikaratasi, kila mmoja anaendelea na shughuli zake katika hali ambayo ni mfano ambao sijaona mahali pengine popote duniani. Nimefurahi sana na nimeridhishwa na vile wananchi walio wapole katika tabia na wanavyokaribisha wageni katika hali ambayo mgeni anajisikia ni kwao. Kwa wanaoishi hapa kwa miaka mingi, ni hakika tabia zao ni bora na zafaa kuwaiga wachina vile wanavyoendesha mambo yao. Mji wa Beijing ni mkubwa sana, ni mji ambao umepangwa vizuri, msafi sana na kila mmoja anaendesha kazi zake bila wasiwasi na hali ya usalama iko juu kabisa.

Mwandishi: Tunaomba utumie fursa hii kuwaambia wasikilizaji wetu walioko barani Afrika hasa Afrika ya mashariki na kati umuhimu wa lugha ya kiswahili katika kufanya mawasiliano, kuongeza urafiki na ushirikiano kati ya wananchi wa Afrika ya mashariki na kati.

Waziri: Ningependa kuwahimiza watu wa Afrika mashariki na Afrika ya kati na sehemu kadha wa kadha za Afrika ambapo lugha ya kiswahili inatumika watumie lugha ya kiswhaili kwa mawasiliano yetu. Katika safari yangu nyingi duniani, kila nchi niendayo watu wa nchi hiyo hutumia lugha yao wenyewe ya kiasilia, na sisi lugha yetu ni kiswali, kwa vile sasa kiswahili kinatumika sehemu nyingi duniani, kwa hakika hakuna haja kuongea lugha nyingine ya kigeni, watu wanaweza kutafsiri mara moja, mawasiliano bora zaidi kati yetu ikiwa sote tuelewa tuongea kitu gani, ni vizuri kwa sisi tutumie lugha ya kiswahili ili tuweze kuendeleza maendeleo yetu katika hali ambayo sote tuelewa tufanya nini na tutapata kitu gani.

Mimi nashukuru sana nafurahi kusikia kuwa lugha ya kiswahili kutumika hapa China, hii inasaidia sana sisi kama waafrika hasa wa Afrika ya mashariki na kati ambapo kiswahili kinatumika kuwa urafiki wetu utaimarishwa zaidi ambalo kwa babu lugha ni moja ya vyombo ambavyo vinatumika katika nchi na kati ya watu binafsi. Asante.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-10


1  2