Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-13 15:52:34    
Maonesho ya muziki wa kitaifa mjini Beijing

cri

Siku chache zilizopita Bendi ya Muziki wa Kikabila ya Redio ya China ilifanya maonesho ya muziki mjini Beijing.

[sauti 1]

Mliosikia ni muziki unaoitwa "Nderemo". Huu ni muziki wa kitaifa wa mtindo wa kusini wa China, muziki huo ulipigwa kwa ala za Kichina ukieleza mila na desturi za watu wanaoishi katika sehemu ya kusini yenye mito mingi. Muziki huo pia uliwahi kupigwa katika maonesho ya muziki katika siku mkutano wa viongozi wa nchi za Asia, APEC, uliofanyika mjini Shanghai mwaka 2000 na nchini Ufaransa wakati Shanghai ilipoomba kuwa mwenyeji wa kufanya maonesho ya kimataifa mwaka 2002.

[sauti 2]

Bendi ya muziki wa kitaifa ya Redio ya China ni moja kati ya bendi kubwa za muziki wa kikbila nchini China. Tokea bendi hiyo ilipoanza kuongozwa na Peng Xiuwen imekuwa maarufu zaidi kutokana na kupiga miziki mingi ya kitaifa. Katika maonesho hayo mziki mwingi uliopigwa ulitungwa na watunzi wakubwa katika miaka ya karibuni

[sauti 3]

Mliosikia ni muziki unaoitwa "nyimbo zasikika kila mahali" uliopigwa kwa filimbi kwa kushirikiana na ala nyingine. Muziki huo umehaririwa kutoka wimbo unaoimbwa sana miongoni mwa watu wa kabila la Wamiao wanaoishi katika sehemu ya kusini magharibi mwa China. Wamiao waliimba wimbo huo miaka hadi miaka na kizazi hadi kizazi, ukionesha jinsi Wamiao wanavyokuwa na furaha katika sikukuu yao.

[sauti 4]

Bw. Tan Tun ni mtunzi mkubwa wa muziki. Mwaka 2000 muziki wake wa filamu ulipata tuzo ya Oscar, alikuwa Mchina wa kwanza aliyepata tuzo hiyo. Kwenye maonesho, bendi hiyo ilipiga muziki wake mwingine wa "tambiko" ambao unaonyesha mazingira ya jinsi tambiko ilivyofanyika katika kasri la kifalme katika China ya kale, muziki huo ulipigwa kwa tarumbeta ya Kichina ikishirikiana na ala nyingine za Kichina, ambao ni muziki wenye muunganisho wa mitindo ya kisasa na ya kale.

[sauti 5]

Katika miaka mingi iliyopita bendi hiyo ya muziki wa kitaifa ilishirikiana na watunzi wengi wa muziki na ilipiga muziki mwingi wa kisasa na wa mtindo wa jadi wa Kichina. Tulipokaribia mwisho wa kipindi hiki tusikilize muziki mwingine uliotungwa na Guo Wenjing, "jua, mwezi na mlima".

[sauti 6]

Mliosikia ni muziki unaoonesha jinsi binadamu wa asili walivyoabudu na kutamani kuishi zaidi. Muziki huo ulichanganya muziki wa makabila madogo madogo ya China na ulipokaribia mwisho ulitumia sauti laini ya kwaya kwa kuchangia mazingira ya kale.

[sauti 7]

Mliosikia ni mziki uliopigwa na Bendi ya Muziki wa Kikabila ya Redio ya China. Kipindi hiki kinaishia hapa. Tunawatakieni wikiendi njema, kwaherini.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-13