Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-13 21:31:03    
Serikali ya China ina nia imara na uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa ukimwi

cri

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao tarehe 13 hapa Beijing alipokutana na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la mipango ya ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa Peter Piot amesema kuwa, serikali ya China ina nia imara na uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa ukimwi. China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na jumuiya za kimataifa ili kutoa mchango katika kinga na tiba ya ukimwi duniani kote.

Waziri mkuu Wen Jiabao amesema, serikali ya China inatilia maanani sana kinga na udhibiti wa ugonjwa wa ukimwi, imetunga sera na mipango ya nchi ya kinga na tiba ya ukimwi, kutumia nguvu kubwa, mali na vifaa kwa kutoa misaada ya lazima na dawa bure kwa wagonjwa wa ukimwi, kutoa upimaji bure kwa watu wanaopenda kupimwa ugonjwa huo, na kuwapatia wajawazito walioambukizwa virusi vya ukimwi dawa za kuzuia maambukizi ya maradhi kwa watoto wachanga, na kuwapa ada za shuleni watoto yatima wa ukimwi.

Amesema kuwa serikali ya China itaendelea kuongeza nguvu ya kinga na tiba ya ukimwi na kuhakikisha hatua zote zinaweza kutekelezwa vizuri.