Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-14 15:16:15    
Mkwaruzano wa biashara ya nguo kati ya China na Ulaya na Marekani

cri

Mkwaruzano uliotokea hivi karibuni wa biashara ya nguo kati ya China pamoja na Marekani na Umoja wa Ulaya umefuatiliwa na pande zinazohusika. Kwanza ni Marekani na Umoja wa Ulaya ziliamua kwa nyakati tofauti kuweka kikomo cha uagizaji wa aina fulani za bidhaa za nguo kutoka China, kisha ni China ambayo ilichukua hatua ya kukabiliana na hatua hizo zilizochukuliwa, na ilipunguza ushuru wa baadhi ya bidhaa za nguo zinazosafirishwa nje na kuufanya mkwaruzano wa biashara ya nguo kupamba moto zaidi. Hata hivyo, hali mpya inaonesha kuwa mgogoro wa biashara ya nguo kati ya China pamoja na Ulaya na Marekani unaanza kupungua, na pande zote husika zimeeleza kuwa hazipendi kuona suala la biashara ya nguo linaathiri uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.

Kutokana na hali ya hivi sasa ya mkwaruzano wa biashara ya nguo kati ya China Ulaya, watu bado hawajaona vizuri manufaa yanayoletwa na hatua inayochukuliwa na Ulaya na Marekani ya kuweka kikomo cha uagizaji kuhusu bidhaa za nguo za China, ndani ya nchi zao zimekuwa na maoni tofauti, lakini athari mpya inayoletwa kwa biashara kati ya China pamoja na Ulaya na Marekani kutokana na kuweka kikomo zimeonekana dhahiri, na ile ya moja kwa moja ni athari mpya kwa sekta ya nguo ya China.

Mkoa wa Zhejiang ulioko sehemu ya mashariki ya China ni wa kwanza kwa uzalishaji wa nguo nchini China, thamani ya bidhaa za nguo zinazosafirishwa kwa nchi za nje za mkoa huo inachukua 20% ya thamani ya bidhaa za nguo za China zinazosafirishwa nje. Kuwekwa kwa kikomo kumeathiri moja kwa moja uzalishaji wa viwanda vya mkoa huo. Kiongozi wa kiwanda kikubwa kabisa cha nguo cha huko bibi Fu Ading alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,

"Hali ya hivi sasa ni kuwa uzalishaji nguo wa kiwanda chetu utapunguzwa kwa nusu, na tena hatuna uhakika na juu ya oda za nguo katika siku za baadaye."

Kiongozi huyo alisema kuwa 90% ya nguo zinazozalishwa na kiwanda chao zinasafirishwa kwenda Marekani na Umoja wa Ulaya, na kuwekwa kikomo na Ulaya na Marekani kwa uchache kutasababisha hasara ya dola za kimarekani milioni 2.

Viwanda vingi ambavyo nguo vinavyozalisha hasa zinasafirishwa nje, pia vinakabiliwa na hali ya namna hiyo. Takwimu zilizotolewa na serikali ya China zinaonesha kuwa sekta ya nguo ya China imeajiri watu zaidi ya milioni 19. Kuwekwa kikomo na Ulaya na Marekani kumeathiri bidhaa zinazosafirishwa nje zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.3 na ajira ya watu zaidi ya laki 1.

Kwa upande mwingine hatua iliyochukuliwa na Ulaya na Marekani ya kuweka kikomo cha uagizaji wa bidhaa ya nguo kutoka China pia haiungwi mkono na wateja. Huko Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji, mwandishi wetu wa habari kwenye supamaketi ya Carrefour alimhoji mteja mmoja bibi Vieginie Denoz, naye alisema,

"Kwa kiwango fulani, ninaona ongezeko la bidhaa za nguo za China zinazosafiriwa katika nchi za Umoja wa Ulaya siyo kubwa sana. Umoja wa Ulaya inajitahidi kuwania biashara huria ya nguo kwa bidhaa zake yenyewe, hivyo Umoja wa Ulaya ungekubali hali ya namna hiyo. Mimi ninaponunua nguo sijali kama nguo hiyo inatoka wapi. Kwangu mimi ninataka kununua nguo nzuri na yenye bei nafuu."

Mambo kama hayo pia yanatokea nchini Marekani, baadhi ya watu walipohojiwa na mwandishi wetu walisema kuwa wanapenda nguo za China, tena hawaamini kuwa tatizo la ajira nchini Marekani linatokana na nguo zilizoagizwa kutoka China. Katika jimbo la New Mexico nchini Marekani mteja mmoja Bw. Carlos Castaneda alisema,

"Hivi sasa bei za baadhi ya bidhaa zinapanda, nguo za bei rahisi za China ni nafuu sana kwa watu wa Marekani. Serikali ya Bush inasema kuwa bidhaa kutoka China zimesababisha ongezeko la upungufu wa ajira. Lakini Mexico na nchi nyingine pia zinasafirisha bidhaa za nguo kwa Marekani, pengine China siyo kitu muhimu sana katika suala hilo.

Baadhi ya wataalam wa uchumi wa China pia hawaamini usafirishaji nguo wa China utaleta pigo kwa sekta ya nguo ya Ulaya na Marekani. Kiongozi wa jumuiya ya sekta ya viwanda vya nguo ya China Bw. Gao Yong alichukua mfano wa Marekani kuweka kikomo kwa bidhaa za suruali za China, alisema kuwa ikilinganishwa na mwaka jana, katika miezi minne ya mwanzo ya mwaka huu, bidhaa ya suruali za China zilizosafirishwa kwenda Marekani ziliongezeka kwa mara 3, lakini suruali za China zinachukua nafasi ya pungufu ya 2% kwenye soko la suruali nchini Marekani, kiasi hiki kidogo hakiwezi kuleta pigo kwa sekta ya ngu ya Marekani.

Bw. Gao Yong alisema kuwa kabla ya miaka 10 iliyopita, mkataba wa nguo wa WTO umeagiza wazi kuwa nchi zilizoendelea zinatakiwa kuongeza mgao wa usafirishaji wa nguo wa nchi za nje hatua kwa hatua katika muda wa miaka 10. Lakini mgao huo ulipofikia kiwango cha 70% hadi 90% ulisimama hadi ulipoondolewa wakati wa mwisho, hali ambayo ilisababisha ongezeko kubwa la bidhaa za nguo kutoka China.

Ingawa China ingenufaika kutokana na haki ya biashara huria ya kuzisafirishia bidhaa za nguo Ulaya na Marekani baada ya kuondolewa mgao wa usafirishaji bidhaa, lakini ili kudhibiti ongezeko kubwa litakalotokea baada ya kuondolewa mgao wa usafirishaji, China ilitangaza kwa mara mbili kuongeza ushuru wa bidhaa za nguo zinazosafirishwa nje, na baadhi ya ushuru wa bidhaa za nguo uliongezeka mara 5 kuliko zamani, ambapo usafirishaji wa bidhaa za nguo ulianza kupungua mwezi hadi mwezi.

Lakini nchi za Ulaya na Marekani bado hazikuridhika na hatua iliyochukua serikali ya China, zikaweka vikwazo. Kwa kufuatia, serikali ya China iliondoa nyongeza ya ushuru wa forodha kwa bidhaa za nguo zilizosafirishwa nje, ambapo mkwaruzano wa biashara ya nguo ukapamba moto.

Jambo linalofurahisha ni kuwa China pamoja na Ulaya na Marekani zimekubali kutatua tatizo hilo kwa njia ya mazungumzo.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-14