Mkurugenzi wa shirika la kupambana na ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS Bw. Peter Piot ambaye yuko ziarani mjini Beijing tarehe 14 aliwatunukia tuzo la kutoa michango maalum katika kukinga ugonjwa wa AIDS waziri wa afya wa China Bw. Gao Qiang na naibu mkurugenzi wa kituo cha kukinga ugonjwa wa ukimwi wa China Bi. Shen Jie.
Katika sherehe ya kutunukia tuzo, Bw. Piot alisema kuwa, serikali ya China inafanya juhudi kubwa na kuweka sera dhahiri kuhusu kazi ya kukinga ugonjwa wa AIDS, na inasifiwa na tume ya AIDS ya Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa.
Bw. Gao Qiang alipokutana na Bw. Piot alisema kuwa, serikali ya China inazingatia sana kazi ya kukinga ukimwi, na kutunga sera nyingi za kupamabana na kuenea kwa ukimwi. Amesema China inapenda kupanua na kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Mataifa, na mashrika mengine ya kimataifa, ili kutoa mchango katika kupambana na ukimwi nchini China na duniani.
|