Katika Chuo Kikuu cha Viwanda Vyepesi cha Dalian, wanafunzi wengi watakaohitimu masomo wanaposhughulika kutafuta kazi, msichana Zhao Qing ameamua kuanzisha shirika lake mwenyewe mjini Dalian. Alisema kuwa, kutokana na utaratibu husika wa kujiajiri kwa wanafunzi waliohitimu chuo kikuu wa mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, baada ya kupata diploma, ataweza kuomba mkopo na kupewa fursa nafuu ya kupunguziwa au kufutiwa kodi husika.
Hivi sasa wanafunzi wengi zaidi na zaidi wa China waliohitimu chuo kikuu wanapenda kujiajiri kwa kuanzisha mashirika yao wenyewe. Habari zinasema kuwa, katika miaka miwili iliyopita, mkoa wa Liaoning umekuwa na wanafunzi waliohitimu chuo kikuu zaidi ya 2000 walioanzisha mashirika yao wenyewe. Mji wa Shenyang, mji mkuu wa mkoa huo tangu utoe huduma za kuanzisha mashirika wenyewe kwa wanafunzi waliohitimu chuo kikuu mwezi Oktoba mwaka 2003, umewakabidhi wanafunzi 168 waliohitimu chuo kikuu "cheti cha kujianzisha shirika", na mashirika yaliyoendeshwa na wahitimu 125 hao yameanza shughuli, na kuweza kutoa nafasi 1360 za ajira, wengi walioajiriwa na mashirika hayo ni wahitimu wa chuo kikuu. Mashirika hayo yaliyoendeshwa na wahitimu hao hushughulikia sekta ya kompyuta, mafunzo ya elimu, upashanaji habari, usanifu wa mapambo ya majengo na nguo na kadhalika.
Serikali za sehemu mbalimbali nchini China kwa nyakati tofauti zimetunga sera husika za kuwasaidia wahitimu wa chuo kikuu kuanzisha mashirika yao binafsi. Mwaka 2003 na 2004, kati ya hatua 70 zilizochukuliwa na serikali ya mkoa wa Liaoning za kuhimiza wahitimu wa chuo kikuu kupata kazi, hatua zaidi ya 20 zinahusiana na wanafunzi kuanzisha mashirika wenyewe, kama vile usimamizi wa usajili wa familia, kupunguza au kufuta kodi, kutoa dhamana ya mkopo na huduma za jamii. Kwa mfano, mashirika yaliyoendeshwa na wahitimu wa chuo kikuu kwenye sehemu zilizoko pembezoni na zenye matatizo ya kiuchumi yatasamehewa ushuru kwa miaka mitatu; kurahisisha taratibu kupata mikopo midogo; na kuwawezesha wapate mafunzo kuhusu jinsi ya kujiendeleza bila malipo yoyote na kadhalika. Mkoa wa Jilin kaskazini mashariki mwa China pia umetunga sera husika za kipaumbele, kuwaunga mkono wahitimu wa chuo kikuu kuanzisha mashirika wenyewe, ambao wamechukuliwa kuwa ni nguvu muhimu ya kuhimiza sekta ya huduma, na mashirika yasiyomilikiwa na taifa katika miji midogo.
Vyuo vikuu vya China vimekuwa vituo vya kuwaandaa wavumbuzi wa kazi. Chuo Kikuu cha Viwanda Vyepesi vya Dalian kuanzia mwaka 2001 kilianzisha somo la uendeshaji wa mashirika madogo. Hadi leo, wanafunzi zaidi ya 500 wamechagua mafunzo hayo, kwa wale wenye nia ya kuanzisha mashirika wenyewe wanapewa muongozo, na wanafunzi wanaotihimu chuo kikuu wenye nia ya kuanzisha mashirika binafsi wanasajiliwa pamoja.
Idhaa ya Kiswahili 2005-06-15
|