Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-16 15:18:37    
Watoto wa China wakua katika mazingira mazuri ya kifamilia

cri

Wazazi wa China wanafuatilia sana kuwapa watoto wao elimu nzuri ya nyumbani, katika miaka ya karibuni, wazazi wengi wamebadili mtizamo wao kuhusu elimu ya nyumbani na kuwalea watoto kwa njia ya kisayansi. Mashirika ya wanawake na watoto na shule za wazazi wa watoto nchini China pia zinajaribu kuwasaidia wazazi kutatua masuala wanayokutana nayo, ili kuwawezesha watoto wao waishi kwa furaha katika mazingira mazuri ya kifamilia.

Msichana anayeimba wimbo huo anaitwa Su Yi, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita la shule ya msingi ya sehemu ya Haiding mjini Beijing. Mwalimu wake alimsifu kuwa ni kijana mwenye afya na akili timamu. Japokuwa matokeo yake ya masomo siyo mazuri kabisa darasani, lakini yeye ni mchangamfu, mwenye imani na anayefurahi kuwasaidia wanafunzi wengine, hivyo anakaribishwa na walimu na wanafunzi wa darasani. Mama yake Bi. Ma Guiling alisema kuwa, tabia yake nzuri inatokana na uhusiano mzuri wenye usawa kati ya wazazi na mtoto nyumbani.

Bi. Ma Guiling alisema kuwa, yeye na mume wake wanabadilishana mawazo na mtoto wao kwa urahisi kutokana na kumchukua mtoto kama rafiki. Wanafamilia wote wanakwenda kutazama filamu na kuimba nyimbo kwa pamoja. Bi. Ma alisema kuwa, japokuwa hayo ni mambo madogo, lakini yanawasilisha upendo na hisia za kifamilia, yatakuwa na umuhimu mkubwa kwa kujenga tabia yenye furaha ya mtoto.

Hivi sasa, nchini China wazazi wengi zaidi wanawaheshimu watoto wao kama Bi. Ma Guiling anavyofanya, kuzidi kubadilishana mawazo na watoto wao, na kuweka mazingira mazuri ya kifamilia kwa watoto.

Lakini siyo rahisi kwa wazazi wote kufanya hivyo. Mawazo ya jadi ya elimu ya nyumbani nchini China yanawataka watoto kuwatii kabisa wazazi wao, kufuatilia zaidi masomoi, na kupuuza umuhimu wa kubadilishana mawazo kati ya wazazi na watoto wao. Hatua kwa hatua baadhi ya wazazi walipata uzoefu wakaanza kufahamu kuwa, watoto wanatakiwa kupewa uhuru kiasi Fulani na fursa sawa ya kufanya mazungumzo, ama sivyo hawawezi kujiendeleza vizuri.

Wakati wa kubadilishana mawazo na watoto, wazazi hukumbwa na masuala mapya. Watoto katika vipindi tofauti vya umri wana masuala tofauti, kama wazazi hawawezi kushughulikia vizuri masuala hayo watakuwa na mgogoro na watoto wao. Hivyo wazazi wengi wa China hujifunza jinsi ya kutatua masuala hayo katika shule za wazazi ya watoto. Hivi sasa China ina shule za wazazi wa watoto zaidi ya laki tatu, pamoja na vituo vingi vya huduma za wazazi mitaani ambavyo vitatoa maelekezo kwa wazazi.

Shule ya wazazi wa watoto ya shule ya sekondari ya Xi'an, mkoani Shangxi, magharibi mwa China inajulikana sana nchini China. Naibu mkuu wa shule hiyo Bi. Wang Lanjun alisema kuwa, shule hiyo inazingatia kuweka masomo tofauti kutokana na rika tofauti ya watoto, kuwafahamisha wazazi jinsi ya kutatua masuala yanayowakabili watoto wao, hivyo inakaribishwa sana na wazazi wa watoto.

Kwa kufanya maingiliano, wazazi wengi wanawasaidia watoto wao kutatua masuala mengi halisi wanayokutana nayo katika mwendo wa kukua, na kuwa na mtizamo sahihi wa kazi, thamani ya vitu na maisha.

Nyumbani ni mazingira ya kwanza ya ukuaji kwa watoto, hivyo kuwawezesha watoto wakue katika mazingira mazuri ya kifamilia kunafuatiliwa sana na wazazi na jamii ya China. Serikali ya China muda si mrefu uliopita ilitoa waraka ukizitaka sehemu mbalimbali zifuatilie elimu ya nyumbani ya watoto . Mashirika ya wanawake na watoto ya China pia yanashughulikia kuhimiza kujenga kwa mazingira mazuri ya elimu ya nyumbani, kwa mfano kuwatunukia baadhi ya wazazi waliofanya vizuri katika kuwaelimisha watoto nyumbani.

Mkuu wa idara inayoshughulikia mambo ya watoto ya shirikisho kuu la wanawake la China Bi. Jiang Yuee alisema kuwa, moja ya kazi zake muhimu ni kuwahimiza wanawake kujifunza jinsi ya kuwaelimisha watoto wao nyumbani kwa njia ya kisayansi. Anasema:

"Sisi tulifanya mkutano maalum kuhusu kazi ya elimu ya nyumbani, kutunga nyaraka kadhaa za maelekezo, kama vile maoni ya maelekezo ya shule za wazazi wa watoto, utaratibu wa vitendo vya wazazi vya kuwaelimisha watoto. Pia tumetunga vitabu vya kiada na kuvisambaza nchini kote ili kuwafundisha wazazi mtizamo wa kisayansi wa kuwaelimisha watoto."

Bi. Jiang alisema kuwa, kabla ya siku ya watoto ya kimataifa ya mwaka huu, shirikisho kuu la wanawake la China liliwatunukia baadhi ya wazazi bora wa watoto waliochaguliwa, na kueneza njia nzuri walizotumia katika kuwaelimisha watoto.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-16