Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-16 21:12:10    
Sehemu muhimu za ardhi oevu nchini China

cri

1. Hifadhi ya kimaumbile ya Zhalong yenye eneo la hekta laki 2.1 iko katika mji wa Qiqihar mkoani Heilongjiang. Katika hifadhi hiyo kuna aina tatu za ardhi oevu, yaani maziwa, vinamasi na malisho, na kuna aina 468 za mimea, aina 46 za samaki, aina 260 za ndege. Korongo ni ndege muhimu wanaohifadhiwa huko.

2. Hifadhi ya kimaumbile ya Xianghai yenye eneo la hekta 105,467 iko katika wilaya ya Tongyu magharibi mwa mkoa wa Jilin. Kuna mito mitatu, maziwa 22 na eneo kubwa la kinamasi. Huko kuna aina 253 za ndege, aina 30 za wanyama, aina 8 za wanyama watambazi, aina zaidi ya 30 za samaki na aina zaidi ya 600 za mimea. Korongo na miti ya Ulmus macrocarpa ni wanyama na mimea muhimu vinavyohifadhiwa huko.

3. Hifadhi ya kimaumbile ya Bandari ya Dongzhai yenye eneo la hekta 3337.6 iko katika wilaya ya Qiongshan mkoani Hainan. Mfumo wa viumbe wanaoishi katika delta za mito, bandari na ufukwe zilizoko kando ya ukanda wa joto wa kizio cha kaskazini na sehemu ya kuishi kwa ndege katika majira ya baridi vinahifadhiwa huko. Kuna aina 26 za miti ya mikoko na aina 40 za mimea inayoishi pamoja na miti ya mikoko, ambavyo zinachukua asilimia 90 ya aina za miti ya mikoko nchini China.

4. Hifadhi ya kimaumbile ya kisiwa cha ndege cha ziwa la Qinghai iko mkoani Qinghai. Urefu wa sehemu hiyo kutoka usawa wa bahari ni mita 3200, na eneo la hifadhi hiyo ni hekta 695,200. Aina 162 za ndege wanaishi huko, ambao wengi wao ni ndege wanoishi majini. Kuna shakwe wenye kichwa cheusi wapatao 9000, mnandi wapato 5000, bata maji wenye kichwa chenye miraba zaidi ya 12,100 na shakwe wenye kichwa kahawia zaidi ya 21,300. Aidha, ndege zaidi ya elfu 70 wanapumzika huko wanaposafiri kupitia sehemu hiyo.

5. Hifadhi ya kimaumbile ya Ziwa la Dongting la Mashariki yenye eneo la hekta laki 1.9 iko mkoani Hunan. Huko kuna aina 159 za mimea yenye mishipa, aina 114 za samaki na aina 158 za ndege. Sehemu hiyo ni sehemu muhimu ya kuishi kwa ndege katika majira ya baridi, ambako kila mwaka ndege zaidi ya milioni 10 wanaishi huko katika majira ya baridi.

6. Hifadhi ya kimaumbile ya Ziwa Boyang iko kaskazini mwa mkoa wa Jiangxi. Aina zipatazo 250 za ndege zinahifadhiwa huko. Na kuna aina 122 za samaki katika ziwa hilo, ambao wengi wao ni wenye thamani ya kibiashara. Na ndege wapatao laki 1 wanaishi huko katika majira ya baridi.

7. Hifadhi ya ardhi oevu huko Mipu na Ghuba ya Houhai mkoani Hongkong ina eneo la hekta 1500. Ndege na sehemu wanakoishi zinahifadhiwa huko.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-16