Katika miaka ya karibuni maji ya barafu ya milimani iliyoyunyuka yamelimbikana kuwa maziwa mengi huko sehemu ya Everest. Uchunguzi wa mwanzo unaonesha kuwa kwa uchache kuna theluthi moja ya maji ya barafu kiasi cha mita za ujazo milioni 30 yamekwama huko sehemu ya juu, hali ambayo imeleta athari kubwa kwa matumizi ya rasilimali ya maji ya kwenye sehemu hiyo.
Kiongozi wa kikundi cha utafiti wa kisayansi Bw. Kang Shichang alisema kuwa upimaji uliofanywa katika miaka ya karibuni unaonesha kuwa sehem yenye barafu milimaji iliyoyeyuka inaendelea kupanuka, barafu inayuyuka kwa haraka, hali ambayo imefanya maji yaliyolundikana sehemu ya juu kuwa maziwa.
Kuweko kwa maziwa ya maji yaliyotokana na barafu ya milimani kuyeyuka ni matokeo ya kubadilika kwa hali ya hewa, katika kipindi cha nne cha kabla ya miaka milioni 2 iliyopita, barafu iliyoko kwenye mwinuko wa milima na mabondde ikichukua mawe madogo madogo ilijiteleza taratibu kwa sehemu ya chini na kuchimba ardhi ya sehemu ya chini, baada ya hali ya hewa kubadilika kuwa joto, barafu ilipungua hatua kwa hatua mpaka kuwa maziwa.
Katika uchunguzi uliofanywa kwenye mlima wa Everest, watafiti walichimba kwa kutumia mitambo wakaona sehemu ya chini ya maziwa hayo ni mawe yasiyovuja maji. Lakini katika muda wa mwezi mmoja hivi maji ya maziwa yalipungua kwa sentimita 30 hadi 40, hivyo wanaona kuwa maji ya maziwa walinywewa na hewa, wakati baadhi ya maji yaliingia kwenye kingo za maziwa.
Kiongozi wa kikundi cha watafiti wa barafu ya milimani kutoka idara ya utafiti wa uwanda wa juu wa Qingzang ya taasisi ya sayansi ya China Bw. Liu Jingshi alisema kuwa data husika inaonesha kuwa kabla ya miaka 40 iliyopita, barafu ya sehemu ijulikayo kwa Rongbu ilipungua na miita za ujazo milioni 100 yaliingia mto Rongbu, lakini uchunguzi na upimaji uliofanywa safari hiyo unaonesha kuwa endapo hali iliyogunduliwa katika uchunguzi wao itaendelea vivyo hivyo, basi kwa uchache theluthi moja ya maji kutoka barafu iliyoyeyuka, yaani mita za ujazo milioni 30, yalikwama katika maziwa na hayawezi kutiririka kwa sehemu ya chini.
Habari zinasema kuwa 60% hadi 70% ya rasilimali ya maji yanatokana na barafu. Bw. Kang Shichang anaona kuwa hali hiyo itaathiri vibaya matumizi ya rasilimali ya maji katika sehemu hiyo, yaani wakati watu wanapohitaji sana maji ya kumwagilia mashamba sehemu ya chini katika majira ya kuchipuka, maji ya barafu hayawezi kujaza pengo hilo, badala yake maji yaliyoko katika maziwa milimani yakibomoa ukingo wa maziwa yatasababisha mafuriko makubwa. Endapo utafiti wao wa mwanzo utathibitishwa, idara husika zinapaswa kukaa macho na kujiandaa vizuri.
Utafiti unaonesha kuwa katika miaka ya karibuni hewa ya dunia kubadilika kuwa joto inafanya maziwa yaliyoko kwenye uwanda wa juu wa Tibet kuwa na maji mengi kwa haraka, na kutokea matukio mengi ya kubomoka kwa kingo za maziwa, ambayo yanaleta maafa kwa wakazi wa sehemu iliyoko chini ya maziwa. Takwimu inaonesha kuwa katika muda wa miaka zaidi ya 60 toka katikati ya miaka ya 30 hadi katikati ya miaka ya 90 ya karne ya 20, kingo za maziwa 13 milimani zilibomoka mara 15 na kusababisha mafuriko ya maji na maporomoko ya udongo na mawe.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-17
|