Ili kuhakikisha usalama wa walimu na wanafunzi, tarehe `6 Wizara ya Usalama wa Umma ya China imechukua hatua nane ikiwa ni pamoja na kupeleka walinzi kwenye shule za msingi na za sekondari na shule za chekechea.
Hivi sasa nchini China kuna shule zaidi ya laki 5.9 zikiwemo shule za chekechea, wanafunzi na watoto katika shule hizo wako milioni 230. Usalama ndani na pembezoni mwa shule hizo ulifuatiliwa sana katika miaka kadhaa iliyopita, na idara za usalama zilifanya kazi nyingi kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa shule hizo. Naibu waziri wa usalama wa umma Bw. Bai Jingfu alisema, "Katika miaka ya karibuni, kwa kushirikiana na idara za elimu na utamaduni, wizara ya usalama ilifanya juhudi nyingi kwa ajili usalama wa shule na sehemu pembezoni, vikundi vingi vya uhalifu ndani na nje ya shule vilichukuliwa hatua na wahalifu wengi waliohujumu wanafunzi walikamatwa. Kutokana na mazingira yalivyo baadhi ya idara za usalama zilipeleka askari polisi wenye uzoefu kutoa mihadhara kuhusu sheria na usalama. Kwa kufanya hivyo wanafunzi wameinua mawazo ya kuzingatia sheria na tahadhari ya kujikinga."
Kutokana na juhudi hizo zilileta hali ya usalama wa shule, wanafunzi na walimu imetengemaa kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo kazi za kuhakikisha usalama bado kuna pengo, kwamba wahalifu waliohujumu wanafunzi bado wapo na kufanya uhalifu ndani na pembezoni mwa shule. Matukio ya wanafunzi kukiuka sheria, kujiua na kukanyagana katika vurumai na kupata sumu kutoka vyakula yanaendelea kutokea, hali ya usalama pembezoni mwa shule pia hairidhiki.
Kutokana na takwimu zisizokamilika, mwaka 2004 matukio ya kuhujumu wanafunzi, walimu na chekechea yalitokea 67 katika mikoa 25, ajali za moto katika shule za msingi na za sekondari na shule za chekechea zilitokea 800. Isitoshe wanafunzi 4,000 walikufa kutokana na ajali za barabarani.
Kwa kufafanua na kutafuta pengo la usalama, Wizara ya Usalama wa Umma ya China imechukua hatua nane. Naibu waziri wa usalama Liu Jinguo alieleza, "Hatua nane za wizara ya usalama ni pamoja na: kuweka watu wenye dhima kwa tukio maalumu; kwa mujibu wa mahitaji watawekwa walinzi katika shule na shule za chekechea; kuweka wasaidizi wa usalama barabarani mbele ya shule; ukaguzi wa kukinga ajali ya moto utafanywa mara moja kwa kila mwaka na kuwaelimisha namna ya kujiokoa katika wakati moto unapotokea, na hatua nyingine."
Naibu wa kwanza wa waziri wa usalama Bw. Bai Jingfu alisema, hatua hizo zitasaidia sana kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa shule za kawaida na shule za chekekea, na usalama pembezoni mwa shule hizo. Imefahamika kuwa wizara ya usalama wa umma imezitaka idara za usalama za kila ngazi ziimarishe mawasiliano na zishirikiane na idara za serikali, za elimu na shule na kuzitekeleza hatua hizo kulingana na mazingira yao. Ili kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa, kuanzia mwezi Julai wizara ya usalama wa umma itashirikisha idara husika kwenda kila mahali shuleni na kusikiliza maoni ya walimu na wanafunzi kuhusu hatua hizo.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-17
|