Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-20 14:21:27    
Mlima Mingyue

cri
Mlima Mingyue uko katika Mji wa Yichun mkoani Jiangxi, mlima huo una vilele 12 ambavyo mwinuko wake kutoka usawa wa bahari ni zaidi ya mita elfu moja. Ukiuangalia mlima huo kutoka mbali, unaweza kuona kuwa kilele chake kikuu ni cha nusu mviringo mithili ya nusu mwezi, hivyo mlima huo ulipewa jina la Mingyue, maana yake ya kichina ni mwezi mwandamo. Katika sehemu hiyo kuna bustani ya misitu ya ngazi ya kitaifa yenye eneo la kilomita za mraba zaidi ya 130.

Watalii hupanda Mlima Mingyue kwa magari madogo ya waya, njia hiyo ya magari madogo ya waya ni yenye mwinuko mrefu zaidi toka usawa wa bahari kuliko nyingine zote za Asia, kupanda magari madogo ya waya kwenda kilele cha mlima kunahitaji dakika 40. Kwenye magari madogo ya waya watalii wanaweza kuona kuwa ukungu mwepesi upo popote bondeni, wakifika tu kwenye kilele cha mlima wataona wazi sura halisi ya mlima huo.

Baadaye watalii hushuka chini ya mlima kwa kutembea kwa miguu, ili njiani waweze kuangalia mandhari kwa kujisterehesha. Mlima Mingyue ni mrefu sana, miti mingi mlimani inaonekana ya kijani zaidi, na maporomoko ya maji ni ya kasi sana yanawavutia zaidi watalii. Watalii wakitembea kwa miguu kwenye njia ya mlimani wanaona utulivu na starehe ya sehemu hiyo na hata wanapenda kung'ang'ania huko.

Mtalii Si Tingting kutoka mkoa wa Shandong alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

Hii ni mara ya kwanza kutembelea sehemu hiyo, nafurahia sana mandhari ya sehemu hiyo, sikuwahi kuona misitu asilia ya namna hiyo, misitu hiyo haikuharibiwa hata kidogo, maumbile yake ya kiasili yanaonekana wazi.

Kwenye Mlima Mingyue kuna vivutio vingi, na vingi vyao vilikuwa na hadithi zao. Kivutio cha Maporomoko ya bonde la mawingu kinawavutia zaidi watalii.

Maporomoko hayo yana mwinuko wa zaidi ya mita 110 toka usawa wa bahari, watu wakiyaangalia kutoka chini yake, wanaona kuwa maporomoko hayo yanaonekana kama dragon mkubwa mweupe anayeruka kutoka mlimani na kujibwaga chini ya mlima, milio ya maporomoko ni kama ngurumo ya radi, na maporomoko yanaifanya sehemu hiyo iwe na manyunyu na ukungu siku zote.

Inasemekana kuwa, katika zama za kale dragon wawili wa maji na moto walifanya vurugu mara kwa mara katika sehemu iliyokaribu na Mlima Mingyue, dragon wa maji alifanya vurugu ndani ya mto, na kusababisha mafuriko makubwa ya mlimani, dragon wa moto alitoa mawimbi ya joto, na ardhi ikawa kame, na mazao ya kilimo hayakuweza kupatikana hata kidogo. Malaika mmoja mbinguni aliambiwa uovu uliofanywa na dragon hao na aliamua kuwaangamiza, akapambana na dragon hao wawili kwa siku 81, mwishoni akamfunga dragon wa maji juu ya mawingu, na kumlazimisha kutoa maji kila siku, maji hayo yakawa "maporomoko ya bonde la mawingu". Na Malaika alichukua barafu kumkandamiza dragon yule wa moto chini ya ardhi, lakini kutokana na mabaki ya joto la mwilini mwa dragon, chemchemi ya maji joto ikatokea mlimani. Mfanyakazi wa sehemu ya chemchemi hiyo Liu Wei alisema:

Chemchemi hiyo iko katika ya ufa wa zaidi ya mita 400 chini ya ardhi katika Mlima Mingyue, joto la maji huwa na nyuzi 68 hadi 72 ya sentigredi, maji yake ni safi sana, hayana rangi wala harufu, yana madini nyingi ya selenium, hivyo yanasaidia sana afya za watu.

Watu wa Yichun wa sehemu ya Mlima Mingyue wakitaja Mlima Mingyue huwa na majivuno makubwa. Dada Jiang Wenfeng alisema:

Sehemu ya Yichun ya Mlima Mingyue ni nzuri sana inapendeza sana, tunataka vijana au wazee wote wakipata nafasi waje kutembelea, watafurahi na kustarehe sana.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-20