Mkurugenzi wa elimu, habari na mawasiliano wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi nchini Tanzania, Dk. Benedict Fimbo alisema kuwa, asilimia 15 tu ya watanzania ndio wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi katika vituo mbalimbali vya ushauri nasaha nchini.
Dk. Fimbo alisema asilimia hiyo ni ndogo, hivyo alishauri jitihada zifanyike kuhakikisha Watanzania wote wanajitokeza na kupima afya zao. Alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi hizo za utoaji huduma ya kupima kwa kuwa imekuwa ikitoa msaada mkubwa.
|