Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-21 18:24:49    
Mkoa ulioko sehemu ya kati ya China watafuta njia ya maendeleo

cri

Mkoa wa Jiangxi, ambao unajulikana kwa maendeleo ya kilimo, ni moja ya mikoa 13 muhimu katika uzalishaji wa nafaka. Katika miaka ya karibuni mkoa huo ukitumia hali bora ya kupakana na mikoa iliyoendelea ya sehemu za mashariki na kusini za China na hali bora yake ya rasilimali na nguvukazi unarekebisha hatua kwa hatua muundo wa uchumi, kujitahidi kushawishi na kutumia mitaji ya kigeni. Wakati mkoa wa Jiangxi unapohimiza maendeleo ya uchumi, unazingatia sana hifadhi ya mazingira ili kupata maendeleo mwafaka ya uchumi na hifadhi ya mazingira.

Hatua moja muhimu iliyochukuliwa na mkoa wa Jiangxi katika kurekebisha muundo wa uchumi ni kuimarisha ujenzi wa maeneo ya ustawishaji wa uchumi na teknolojia na ya ustawishaji wa teknolojia ya kisasa na kuongeza nafasi ya sekta za uzalishaji wa viwanda na sekta ya huduma katika uchumi wa mkoa. Ujenzi wa maeneo hayo ya ustawishaji ni kutenga maeneo na kufanya ujenzi wa miundo mbinu kwenye maeneo hayo maalumu huku serikali inabuni sera nafuu ili kuvutia uwekezaji wa nchi za kigeni na kuhimiza maendeleo ya uchumi.

Eneo la ustawishaji wa sekta ya uzalishaji wa teknolojia ya kisasa la Nanchang ni moja ya eneo la ustawishaji la ngazi ya taifa. Namchang ni mji mkuu wa mkoa wa Jiangxi. Mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano kwenye eneo hilo la ustawishaji aliona, eneo hilo lenye kilomita za mraba 32 lina karakana kubwa za kisasa, barabara pana pamoja na huduma kamili za ushuru, kodi na mambo ya fedha. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya eneo la ustawishaji Bw. Zhang Xiaogang alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa hivi sasa eneo la ustawishaji la Nanchang lina viwanda karibu 800 vya China na nchi za kigeni hususan ni vya mawasiliano ya habari ya elektroniki, software na dawa. Mwaka 2004 pato la eneo hilo lilifikia Yuan bilioni 13. Bw. Zhang Xiaogang alisema kuwa mbali na ujenzi wa miundo mbinu eneo la ustawishaji la Nanchang linatoa huduma bora kwa kampuni za nchi za nje zinazowekeza huko.

"Mara tu baada ya kampuni ya kigeni kuamua kuwekeza huko, inapewa huduma nzuri, licha ya hayo kila mwezi tunaitisha mkutano wa uratibu kuhusu miradi mikubwa inayojengwa kwenye eneo hilo, ambao unapendwa sana na wawekezaji."

Eneo la ustawishaji la Nanchang, ambalo lilianzishwa mwaka 1991, ni moja wa maeneo ya ustawishaji zaidi ya 100 katika mkoa wa Jiangxi. Kutokana na miundo mbinu na huduma bora za eneo hilo pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya miji na tarafa za mkoa wa Jiangxi, eneo la ustawishaji la Nanchang limechukua nafasi ya kwanza mwaka 2004 kwa idadi ya miradi iliyowekezwa, kiasi cha mitaji ya nje na mitaji ya nje iliyotumiwa halisi katika mikoa 6 ya sehemu ya kati ya China.

Hatua nyingine iliyochukuliwa na mkoa wa Jiangxi katika kurekebisha muundo wa uchumi ni kujifunza teknolojia na uzoefu bora wa nchi za nje, ili kuongeza ubora na ufanisi wa uchumi wa mkoa. Habari zinasema kuwa hivi karibuni mkoa wa Jiangxi ulipeleka ujumbe kwenda Hong Kong kufanya shughuli za kuvutia uwekezaji katika miradi ya sayansi na teknolojia, elimu, utamaduni na mambo ya afya, ambapo waliafikiana na wawekezaji kwenye mapatano 67 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.1. Naibu mkuu wa mkoa wa Jiangxi Bw. Wu Xinxiong alisema,

"Tulifanya uchambuzi kuhusu miradi hiyo 67, ambayo kila mradi unafuatiliwa na ofisa mmoja, anawajibika kuushughulikia na kuhimiza utekelezaji wake. Ushirikiano ni wa kati ya watu na watu, hivyo serikali inatakiwa kuaminiwa na wafanyabiashara na kuaminiwa na wananchi."

Ujenzi wa miradi mingi iliyowekezwa si kama tu imechangia maendeleo ya mkoa wa Jiangxi, bali pia umeleta athari mbaya kwa mazingira ya mkoa huo, lakini suala hilo limezingatiwa sana na idara husika ya mkoa wa Jiangxi. Katika miaka ya karibuni mkoa wa Jianxi ulitathimini mara kwa mara uzoefu na mafunzo katika ujenzi wa uchumi na kuimarisha hatua kwa hatua hifadhi ya mazingira ya asili.

Hivi sasa mkoa wa Jiangxi unazingatia sana maendeleo mwafaka ya uchumi na hifadhi ya mazingira, unaona kuwa maendeleo ya uchumi yanatakiwa kwenda sambamba na hifadhi ya mazingira. Ofisa

Hatua nyingine iliyochukuliwa na mkoa wa Jiangxi katika kurekebisha muundo wa uchumi ni kujifunza teknolojia na uzoefu bora wa nchi za nje, ili kuongeza ubora na ufanisi wa uchumi wa mkoa. Habari zinasema kuwa hivi karibuni mkoa wa Jiangxi ulipeleka ujumbe kwenda Hong Kong kufanya shughuli za kuvutia uwekezaji katika miradi ya sayansi na teknolojia, elimu, utamaduni na mambo ya afya, ambapo waliafikiana na wawekezaji kwenye mapatano 67 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.1. Naibu mkuu wa mkoa wa Jiangxi Bw. Wu Xinxiong alisema,

"Tulifanya uchambuzi kuhusu miradi hiyo 67, ambayo kila mradi unafuatiliwa na ofisa mmoja, anawajibika kuushughulikia na kuhimiza utekelezaji wake. Ushirikiano ni wa kati ya watu na watu, hivyo serikali inatakiwa kuaminiwa na wafanyabiashara na kuaminiwa na wananchi."

Ujenzi wa miradi mingi iliyowekezwa si kama tu imechangia maendeleo ya mkoa wa Jiangxi, bali pia umeleta athari mbaya kwa mazingira ya mkoa huo, lakini suala hilo limezingatiwa sana na idara husika ya mkoa wa Jiangxi. Katika miaka ya karibuni mkoa wa Jianxi ulitathimini mara kwa mara uzoefu na mafunzo katika ujenzi wa uchumi na kuimarisha hatua kwa hatua hifadhi ya mazingira ya asili.

Hivi sasa mkoa wa Jiangxi unazingatia sana maendeleo mwafaka ya uchumi na hifadhi ya mazingira, unaona kuwa maendeleo ya uchumi yanatakiwa kwenda sambamba na hifadhi ya mazingira. Ofisa wa mji wa Yichun wa mkoa huo Bw. Liu Mi alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa hapo mwanzoni hawakuzingatia hifadhi ya mazingira, waliwahi kuingiza baadhi ya miradi yenye uchafuzi mwingi vikiwemo viwanda vya saruji, zana za ujenzi na betri.

"Mwanzoni hatukuwa na uchaguzi kuhusu viwanda vilivyowekezwa wala kufikiria uchafuzi kwa mazingira. Hapo baadaye tulifahamu suala hilo, uendelezaji wa viwanda sharti kuzingatia suala la uchafuzi."

Mwaka 2004 pato la mji wa Nachang lilikuwa na ongezeko la 16%, na 40% ya ardhi ya mji mkuu wa mkoa iliyopandwa miti na majani. Wanasema kuwa kanuni moja muhimu ni kukataa ujenzi holela, mazingira ya asili lazima yahifadhiwe wala siyo kuyaboresha baada ya mazingira kuharibiwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-21