Mahitaji
Samaki utepe gramu 500, vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi kila moja gramu 20, mchuzi wa soya vijiko 2, siki vijiko 2, mvinyo wa kupikia kijiko 1, sukari kijiko 1, mafuta gramu 500, mafuta ya ufuta kijiko kimoja
Njia
1. ondoa kichwa, mkia na utumbo, na uioshe na kisha ikate iwe vipande vyenye urefu wa sm 10, viweke ndani ya bakuli moja tia mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya na siki, kisha korogakoroga.
2. tia mafuta ndani ya sufuria pasha moto mpaka yawe na joto nyuzi asilimia 80, tia vipande vya samaki, vikaange kwa dakika 2 mpaka viwe na rangi ya hudhurungi, kisha vipakue.
3. pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, koroga koroga, tia vipande vya samaki, mimina mvinyo wa kupikia, siki, mchuzi wa soya na maji kidogo, na tia sukari korogakoroga, baada ya kuchemka, punguza moto kidogo endelea kuchemsha kwa dakika 5, mimina mafuta ya ufuta, koroga vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|