Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-30 21:47:12    
Michoro ya China

cri

Sanaa ina uhusiano wa karibu na shughuli za uzalishaji za binadamu. Wachina wa makabila mbalimbali kwa busara zao walianzisha sanaa mbalimbali, zikiwemo sanaa za mapango, ujenzi, maandiko, michoro, ufinyanzi na uchongaji. Sanaa hizo zimestawisha hazina ya sanaa na kuwa ustaarabu wa sanaa duniani, pia zimeonesha utamaduni wa jadi na urithi mkubwa wa sanaa wa China.

Katika miaka elfu 5 iliyopita, mapambo yaliyochorwa kwenye vyombo vya udongo vimeonesha jamii ya kale na hisia za wasanii wa kale.

Sanaa ya zamani zaidi ni michoro iliyoko kwenye miamba. Michoro hiyo iligunduliwa katika eneo kubwa nchini China, pamoja na mikoa ya Sichuan, Yunnan, Guizhou, Fujian kusini mwa China na Mlima wa Yinshan, Heihe, Mlima wa Altai kaskazini mwa China.

Picha ya mtu, dragoni na finiksi ni picha iliyochorwa kwenye hariri, iligunduliwa katika kaburi la dola la Chu la Enzi ya Madola ya Kivita, na ni mchoro wa kale zaidi uliogunduliwa nchini China. Kabla ya karatasi kuvumbuliwa, picha zilizochorwa kwenye hariri zilipata maendeleo makubwa na zilistawi sana katika Enzi ya Han ya Magharibi.

Enzi za Wei, Jin, Enzi za Kusini na Enzi za Kaskazini ni kipindi muhimu katika historia ya uchoraji nchini China. Kutokana na vita vilivyodumu kwa miaka mingi na mabadiliko mengi ya uongozi, wanavyuo walitoa mawazo mbalimbali ya kinadharia, ambayo yalisukuma mbele maendeleo ya sanaa. Michoro kwenye ukuta, uchongaji kwenye mawe na michoro ya vanishi vyote vilistawi sana.

Mchoraji mashuhuri Wu Daozi aliyeishi katika Enzi ya Tang ni mchoraji anayechora picha nyingi. Picha zake huonesha hadithi za Dini ya Kibudha na Dini ya Kidao, pia alichora picha kuhusu mandhari, maua, ndege na wanyama. Enzi ya Tang ni kipindi ambacho michoro ya watu ilipostawi. Wachoraji Zhang Xuan na Zhou Fang waliochora picha nzuri kuhusu wanawake waishio katika kasri walikuwa na athari kubwa kuhusu michoro ya wanawake nchini China.

Picha ndefu iitwayo kando ya mto katika sikukuu ya Qingming ilichorwa na mchoraji Zhang Zeduan wa Enzi ya Song ya Kaskazini. Picha hiyo imeonesha mandhari na hali ya pilikapilika za mji mkuu wa Enzi ya Song ya Kaskazini katika sikukuu ya Qingming, na ina athari kubwa kwa utafiti wa historia.

Michoro ya mafuta ni aina ya michoro iliyoingizwa kutoka nchi za magharibi katika Enzi za Ming na Qing. Mwanzoni mwaka karne ya 20, wachoraji wengi wakiwemo Li Shutong, Li Tiefu, Chen Baoyi, Xu Beihong, Lin Fengmian, Liu Haisu walikwenda nchi za nje kujifunza uchoraji wa kutumia rangi za mafuta, na waliingiza ustadi wa uchoraji huo wa Ulaya nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-30