Kuanzia tarehe 10, ujumbe kutoka Zanzibar Tanzania ukiongozwa na waziri wa nchi katika ofisi ya waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna ulifanya ziara ya wiki moja hapa nchini China. Ukiwa hapa Beijing ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea Radio China kimataifa, kituo cha televisheni cha taifa CCTV na Shirika la habari la China Xinhua. Walipokuwa hapa Radio China kimataifa, mtangazaji wetu alipata fursa ya kumhoji Mheshimiwa Shamjhuna.
Mtangazaji: Naomba utuelezee lengo hasa la hapa China pamoja na ujumbe wako.
Mheshimiwa: Nafurahi kupata nafasi hii ya kuongea kwenye Radio China kimataifa. Ujumbe wangu nimekuja na kuongoza ni ujumbe wa watu wanne, akiwemo naibu katibu mkuu, mkurugenzi wa habari na maelezo na kaimu mkurugenzi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar pamoja na mimi mwenyewe. Madhumuni makubwa ya ziara yetu hii ni kuja kuimarisha mashirikiano ambayo tayari yapo, lakini yapo katika sekta ya juu, yaani serikali kwa serikali, sasa tunataka kuanzisha uhusiano wa kivitendo kati ya Radio China kimataifa na Radio Tanzania Zanzibar. Kuna mambo mengi tukayaanzisha na tukayaendeleza katika sekta hii ya habari, hayo ndiyo madhumuni makubwa ya ujio wangu na ujumbe niliokuja nao. Nimefurahi sana kwamba tumepokelewa vizuri, ratiba tuliyokusudia kuitekeleza ilifikishwa hapa mapema, na wenyeji wetu tukawakuta wanajitayarisha na wametutengenezea ratiba ambayo inatufanya tuwe na harakati kila siku, lakini pia inatufanya kufikia malengo tuliyokusudia.
Mtangazaji: Ungefafanua kidogo haya mambo ambayo ya ushirikiano ambayo umekuja kwa ajili ya ushirikiano kati ya Tanzania Zanzibar na China kwenye mambo ya utangazaji.
Mheshimiwa: Kama nilivyosema kuwa kuna mashirikiano ya muda mrefu sana, labda tukienda kwenye historia nyuma kabisa huko utakuta hata wale wasafiri wa kilimwengu wa China. Walifika katika Afrika ya mashariki na walipita Zanzibar pale na baadhi ya vizazi vile ambavyo vinatoka katika ukoo huo. Pale Zanzibar vipo, na sasa hivi wamekuwa nadhani ni kizazi cha nne iko pale Zanzibar na idadi ya watu isiyopungua watu 100 wa China. Kule Zanzibar wako wengi, kuna familia, kuna mtaa na kuna mambo chungu nzima ya kichina. Kwa hivyo uhusiano wetu umeanza zamani , lakini uhusiano wa kisiasa na kiuchumi umeanza mara tu baada ya mapinduzi ya mwaka 1964, ambapo China ilikuwa ni moja kati ya nchi zilizotangulia kutambua mapinduzi ya Zanzibar, na kutoa misaada mbalimbali, ujenzi wa kujenga miundo mbinu, na kuanzisha uchumi wa kisasa, kwa hivyo serikali ya China na Tanzania Zanzibar zina uhusiano wa muda mrefu sana. Sasa tumekuwa na uhusiano wa kitaalamu, na kubadilishana wataalamu kati ya wizara ya afya ya China na wizara ya afya ya Zanzibar. Lakini vilevile kuna uhusiano wa muda mrefu kwenye kituo chetu cha Radio Tanzania Zanzibar. Kwa mfano, kutoka miaka ya 70, serikali ya China ilitusaidia sana kujenga jengo jipya; katika miaka ya 80 ilitusaidia kujenga jengo jipya la studio ya Sauti Unguja pale Zanzibar, na kuanzia hapo wametoa vifaa mbalimbali, na kuanzisha mpango wa kubadilishana watangazaji, kati ya watangazaji wa Zanzibar waliokuja katika idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa, nakumbuka mtu wa kwanza aliyekuja ni mtangazaji wetu Gusaideli. Halafu katika miaka ya 70 akafuatia mtangazaji wetu Suleiman.
Sasa tukiangalia historia hiyo na tukiangalia tulivyodumisha hayo mashirikiano kati ya serikali ya China na serikali ya Zanzibar katika idara ya afya na idara ya habari, tumeona uhusiano wetu tulishusha chini zaidi kwa utendaji.Tuje sasa uhusiano wa kisekta, badala ya uhusiano wa kiserikali tumeona tuko katika uhusiano wa kisekta, ili kuufanya ule uhusiano wa serikali uliopo uwe mzuri zaidi, una nguvu zaidi, na unazaa matunda mazuri zaidi. Kwa maana hiyo, kama tukianzisha sasa mashirikiano katika kuandaa vipindi, tukianzisha mashirikiano katika nyanja za kutoa taarfia za habari, huko ndiko tulikokusudia, tumefikia kwenye makubaliano ya msingi ya mambo manne, tumekubaliana kwamba jambo la mwanzo, Zanzibar kwa kupitia idara yake ya mtandao ya mawimbi, inaweza ikatoe mawimbi kuipa Radio China kimataifa vipindi pale kwa muda wa masaa mawili, tumekubaliana, kwa mfano saa moja watatuia kwa idhaa ya kiswahili, na saa moja kwa kutumia lugha ya kiingereza. Na pia jambo la pili tumekubaliana kwa sababu kuwa mtambo wa kurusha matangazo ambao serikali ya China imeisaidia serikali ya Zanzibar, tunaweza mtambo huo tukautumia kwa pamoja sasa na serikali ya China iongezwe nguvu ule mtambo wa FM na ule wa short wave, ili katika matangazo yatakayofanywa na Radio China kimataifa katika masaa mawili, matangazo yale yaweze kufikia maeneo mengi sana ya Zanzibar, ya Tanzania bara na hata Afrika ya mshariki. Hilo ndilo lengo letu la pili. Lengo la tatu tunazungumzia kurejesha utaratibu wa kubadilishana wataalamu, hii itatusaidia watu wa pande mbili. Zanzibar ina vivutio vikubwa sana vya utalii ambavyo watalii wa China bado hawajavijua, katika mtandao wa namna hii na katika mashirikiano ya namna hii, nchi zote mbili zitanufaishana.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-15
|