F: Ningependa uzungumzie jinsi uhusiano kati ya Watanzania na wachina ulivyo katika kipindi hiki, sijui unaweza kuuelezea vipi.
W: uhusiano na Tanzania maana hii sasa ni la jumla, nikisema Watanzania nasema pia na wa Zanzibar. Uhusiano wa sasa hivi, unakwenda katika nyanja mbili. Uwanja mmoja ulikuwa tumeianzisha kwenye siasa, tumeweka msimamo mzuri sana katika siasa, tumeweka msimamo mzuri sana katika itikadi za kuiendesha nchi, na tumeweka msimamo mzuri sana katika ukombozi, ukombozi wa Zanzibar umesaidiwa sana na harakati za akina Mao Tse Dong, na kujua kwamba kumbe ukombozi ni kazi ngumu, ni kazi ya kujitolea, na ndiyo kwa Zanzibar kwa kufuata utaratibu wa Mao, kwa kufuata msimamo wa kisoshalisti, tuliweweza kuiangusha serikali ya sultani kwa haraka sana, ambayo serikali iishi kwa mwezi mmoja tu baada ya kabidhiwa madaraka na wakoloni wa Uingereza, kwa sababu tulikuwa watu wa kujitolea. Sasa tumekwisha jikomboa, hatujabaki na harakati za ukombozi, maana ukombozi ulimalizikia pale ambapo umekamata nchi ukiwa umeshajikomboa, sasa unakwenda katika uchumi, na katika ustawi wa jamii. Katika hilo mahusiano ya sisi Watanzania na Wachina yameanza zamani. Kwa mfano, ujenzi wa reli ya kuunganisha Tanzania an Zambia, watu wa magharibi waliuchukulia kama ni ujenzi reli ile ni kisiasa, labda ni kupeleka athari ya kisoshalisti kutoka Tanzania na kuisambaza Afrika ya kati. Lakini, haikuwa hivyo, wenzetu wachina waliona kwamba reli ile ina ukombozi wa kiuchumi, kwa sababu nchi za Zimbabwe, Zambia, Malawi, ni nchi ambazo zimo ndani hazina bandari, hazina bandari zilikuwa zinatumia zaidi bandari ya Tanzania kama moja katika milango yake ya kwenda nje, ya kusafrisha bidhaa na biashara kwa ujumla, sasa sisi tulipowaeleza ndugu zetu wa kichina kwamba, tunataka msaada wa kujenga reli hii, wao waliona kwamba, reli hii si tu kuweka mkazo katika suala la kisiasa na ujamaa, lakini pia ilikuwa lina umuhimu kubwa katika kiuchumi, wao wenzetu walikubali kutusaidia yaani ambapo watu kutoka magharibi walikataa kutusaidia. Tukija kwa upande wa Zanzibar, wachina wanakuja kutuanzisha pale Zanzibar, ukulima wa mpunga ukitegemea maji, yaani umwagiliaji wa kutegemea maji na sio kuchimba chini, lakini hata kuchimba chini, vile vile tulianzisha mpango huo, na watu wa kichina, wakaleta ile mfumo wa ujamaa wa kulima mpunga katika kipindi hicho, kwa kweli tulipiga hatua kubwa sana, nayo hiyo ina sehemu ya kiuchumi, maana kwa lugha nyingine tulikuwa tunakuza import subtitution, badala ya kuagizia michele, kutumia fedha za kigeni, tunaweza kulima mpunga, na tukafika lengo la 90% kujitosheleza, na kwa hivyo, tumepunguza uagizaji wa chakula, na tumeweka hela zetu za kigeni, kwa kufanya mambo mengine makubwa ya kujenga barabara, ya kujenga skuli, ya kujenga hospitali, n.k. lakini upande wa maendeleo ya jamii, wachina mpaka leo, tuna mahusiano kwa kubadilisha madaktari wa kutusaidia, na tunakwenda vizuri. Sasa tumeingia katika mtandao wa uchumi wapamoja, yaani utandawazi, uchumi wa pamoja unataka mashirikiano ya karibu, mkubwa na mdogo, kwa sababu tusipofanya hivyo, ule muda wa sasa hivi wa vita baridi haupo, cvita bardidi iligawa ulimwengu katika makundi mawili, la mgharibi na la mashariki, Magharibi walikuwa na nguvu sana za kivita na kiuchumi, lakini mashariki nao walikuwa na nguvu za kivita na kiuchumi, kulikuwa hakuna ambaye alikuwa anatarajia kumwonea mwenziwe, kwa hivyo katika kipindi kile, watu, mataifa yalikuwa yakiishi kwa kuogopana. Baada ya vita vya dunia kumalizika, sasa kuna kitu kinaitwa dunia ya ncha moja, sasa hiyo ina wakubwa ambao hawadhibitiwi, ni wakubwa ambao wanaamua mambo yao, wanatekeleza, bila wengine hata kufuata sheria za kimataifa. Sasa tunazungumzia utandawazi wa uchumi, tunazungumzia soko huria, lakini wenzetu wanaweka vikwazo vya kusema wewe unaruhusiwa idadi fulani tu kuuza kwenye soko letu, wanaweka vikwazo kwa kusema kwamba, ok, bidhaa yako ikija tutaitoza ushuru kiasi fulani, na ushuru kuwa mkubwa, ile bidhaa yako ikiingia kwenye soko isipate kununulika, inakuwa ni ghali, lakini vilevile wanaweka vikwazo vingine vya kutoa ruzuku kwa wakulima wao ili wakulima wao waweze kuuza mazao yao kwa bei rahisi. Sisi huku nchi za Afrika na nchi za Asia, na China ni moja katika nchi za Asia, tusipoungana, tukawa kitu kimoja na tukashirikiana, hawa jamaa waatumaliza kiuchumi, na ukimalizika kiuchumi, maana yake utawala unarudi kwa mlango wa nyuma. Ukitawliwa kiuchumi, maana yake ndiyo umetawaliwa kimawazo, kama kuna wakati tulikuwa tunahitaji mashirikiano ya ukombozi, sasa tunahitaji mashirkiano ya kiuchumi. Mashirikiano ya kiuchumi hayawezi kupatikana kama hakuna mtandao wa taarifa za habari. Taarifa za habari ndizo zitakazokupa sasa kuelewana zaidi kuimarisha maelewano yetu, na kujua kwamba biashara kumbe inaweza ikafanywa hivi, Tanzania wanaweza wakatoa hiki, Zanzibar wanaweza kutoa hiki, sasa tukija katika ile jumuiya ya kimataifa, yaani WTO, tukikaa pamoja kwa kuelewana, wale wakubwa, wanaviwanda, tutawalazimisha kuingia katika mikataba ya biashara, ambayo italeta hali sawa ya ushindani. Tusiposhirikiana, kila mmoja akafuata njia yake, ndiyo tutakuwa tumeumia zaidi.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-22
|